George-Chicken-Lwandamina; Anayetarajia kuchukoa mikoba ya Mholanzi Hans van der Pluijm.
|
Na Mwandishi Wetu
YANGA inatarajia kubadilika
mara utakapomalizika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara Novemba 6
mwaka huu baada ya uongozi kutaka kubadili benchi lote la ufundi la timu hiyo,
imedokezwa.
Kimsimamo wa Ligi Kuu
Tanzania Bara, Yanga iko katika nafasi ya sita baada ya kujikusanyia pointi 11
kufuatia kushuka dimbani mara sita nafasi ambayo haijaufurahisha uongozi wa
klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani.
Taarifa kutoka ndani ya
Yanga zinasema kuwa benchi lote la timu hiyo litaondoka na kuja sura mpya
ikiongozwa na kocha Mzambia, George Lwandamina atakayesaidiwa na Charles
Mkwassa, Manyika Peter kama kocha wa makipa na meneja Sekilojo Chambua.
Kocha Mkuu Hans van der
Pluijm raia wa Uholanzi na wasaidizi wake, Juma Mwambusi, kocha wa makipa Juma
Pondamali na Meneja Hafidh Saleh wote wazalendo wataondoka.
“Mazungumzo yanaendelea,
tutakapokubaliana atakuja kusaini,”kilisema chanzo hicho cha ndani.
Na kuhusu watendaji wapya wa
benchi la Ufundi wazalendo, chanzo kimesema; “Hao wote wamependekezwa
na kwa kuwa ni watu wetu, ni suala la kuzungumza nao tu,”.
Pluijm amejikuta katika
wakati mgumu baada ya Yanga kuambulia pointi 11 kati ya 18 za mechi sita za
Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga SC imetoa sare mbili,
imefungwa mechi moja na kushinda tatu tangu kuanza kwa Ligi Kuu – hiyo ikiwa
ni mbali na kupoteza mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC kwa penalti 4-1
baada ya sare ya 2-2.
Na baada ya mchezo wa Oktoba
1, wakalazimishwa sare ya 1-1 na mahasimu wao, Simba waliokuwa pungufu kwa
sehemu kubwa kufuatia kutolewa kwa kadi nyekundu kwa nahodha wao, Jonas Mkude katika
dakika ya 29, baadhi ya viongozi wa Yanga wamependekeza mwalimu huyo aondolewe
No comments:
Post a Comment