NEW YORK, Marekani
MGOMBEA wa kiti cha Urais wa Marekani kwa tiketi ya
Chama cha Republican Donald Trump (pichani) amesema kwamba yuko tayari kukubali matokeo
ya uchauzi huo “endapo tu atashinda”.
Aliongeza kuwa atakubali "matokeo safi”, lakini
atakuwa na haki ya kuhoji matokeo, ambayo atahisi kuwa na figisu figisu
Trump aliyasema hayo wakati wa mkutano wa kampeni
huko Delaware, Ohio, ambako alizungumza kwa mara ya kwanza kabisa tangu
alipomaliza mdahalo wa tatu na wa mwisho wa wagombea urais uliofanyika alfajiri
ya leo Alhamisi.
Mombea huyo alijikuta matatani wakati wa mdahalo huo
baada ya kusema kuwa kamwe hatakubali matokeo ya uchaguzi huo.
Meneja wa kampeni wa Trump, Kellyanne Conway, baadae
alisisitiza kuwa mombea wake alikuwa na maana kuwa hatakubali hadi pale “matokeo
yatakapojulikana wazi”.
Maelezo hayo, yaliibua hasira kutoka kwa baadhi ya wanachama
wa Republicans, ikiwa ni marudio ya
maelezo ya Trump aliyedai kuwa uchaguzi huo umejaa mizengwe dhidi yake.
Trump aliwaambia wasikilizaji hao wa Ohio kuwa
uchaguzi huo ulikuwa ukizua maswali mengi kuhusu "haki ya nchi hiyo ".
"Kwa kweli napenda kuahidi wapia kura zanu wote
na wafuasi wangu na watu wote wa Marekani, kuwa nitakubali matokeo ya uchaguzi
huu mkubwa na wa kihistoria bila shaka yoyote-endapo nitashinda,”alisema.
Baadae aliongeza: "Nitakubali matokeo ya
uchaguzi safi, lakini pia nitakuwa na haki ya kufunguia kesi ya kuhoji matokeo
hayo."
No comments:
Post a Comment