Na Mwandishi Wetu, Kilwa
TAMASHA la Kwanza la Chakula na Uvuvi lilikamilika
leo usiku a maneno mjini Kilwa Masoko huku bendi ya La Rhumba ikipamba kwa
kupiga nyimbo kibao zikiwemo zile za Kilwa Jazz Band.
Kwa mujibu wa mratibu wa tamaha hilo, ambaye pia
ndiye mmiliki wa Kilwa Dreams Resort Hotel Gradys Rutihinda, tamasha hilo pia ni
kwa ajili ya kupiga vita uvuvu haramu pamoja na kumuenzi mwanamuziki mkongwe
nchini Hemed Kipande, ambaye alikuwa mwenyeji wa Kilwa Kivinje.
Rutihinda alisema kuwa pia tamasha hilo ambalo litakuwa
likifanyika kila mwaka ni kwa ajili ya kutangaza fursa za utalii na uchumi
zilizopo Kilwa, ambazo wengi hawajui kama zipo.
Tamasha hilo limeanza kwa kishindo na kushirikisha
watu kadhaa huku shindano la uvuvi likiwa kivutio baada ya timu ya Kilwa Dreams
kuibuka washindi baada ya kumvua samaki mwenye uzito wa kilo 28 aliyeshinda
timu zingine, huku timu ya Pakaya Ocenic ikimaliza ya pili kwa kumvua samaki
mwenye kilo 12.
Nyama choma ilikuwepo katika tamasha hilo la Chakula na Uvuvi. |
Mchezo wa uvuvi ushirikisha timu yenye watu kadhaa
ambao huenda bahari wakiwa na boti na kuvua samaki kwa kutumia mshipi na
ndoano, uvuvi ambao ni salama kabisa kwa samaki hasa ukizingatia kuwa moja ya
lengo la tamasha hilo ni kupiga vita uvuvi haramu.
Tamasha hilo lilikamilika kwa burudani kutoka kwa La
Rhumba Band pamoja misosi ya nyama choma, ambayo ilipikwa kifundi na wapishi
waliobobea kama Mr. Peter na wengine.
Mmoja wa waratibu wa tamasha hilo, Gradys Rutihinda akiwa amelinyanyua juu Kombe la ushindi wa kwanza wa uvuvi. |
Rutihinda aliwashukuru watu wote waliofika katika
tamasha hilo na kuahidi kufanyika kila mwaka na kuliboresha siku hadi siku na
kuvutia watu wengi zaidi huku akitoa wito kwa wadhamini kujitokeza kwa wingi
kudhamini tamasha hilo.
Alisema mwaka huu wameliendesh wenyewe kwa gharama
zao, ambapo aliwaomba wadhamini kujitokeza ili kumuunga mkono katika harakati
zake za kutangaza fursa zilizopo Kilwa na kumuenzi Kipande.
Tamasha hilo lilifanyikia Kilwa Dreams Resort Kilwa Masoko karibu na pale alipokubwa samaki
mkubwa zaidi kuwahi kuonekana mwenye tani 40, urefu wa futi 45 mwnye mbavu
kubwa mithili ya mkono wa mtu mzima pamoja na mafuta mengi yanayodaiwa kuponya
magonjwa mbalimbali.
Akitanggaza matokeo ya washindi wa uvuvi wa samaki wakati wa tamasha hilo. |
La Rhumba Band ikikonga nyoyo za wapenzi wa muziki wakati wa tamasha hilo. |
Samaki akipimwa ili kujua uzito wake kamili katika shindano la uvuvi wakati wa tamasha hilo. |
Wapenzi wa muziki wakiselebuka wakati La Rhumba ikitumbuiza. |
No comments:
Post a Comment