Kikosi cha Manchester United. |
MANCHESTER, England
KIKOSI cha Manchester United huenda kisibadilike kutoka
kile kilichoshinda mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA wakati timu hiyo
Jumapili itakapokutana na `bingwa’mteule
wa Ligi Kuu Leicester.
Wachezaji kama Luke Shaw, Bastian Schweinsteiger na Will
Keane wataendelea kubaki nje ya uwanjani katika pambano hilo la aina yake.
Leicester City wenyew watajaribu kutwaa taji hilo la
Ligi Kuu bila ya kuwa na mshambuliaji wake hatari Jamie Vardy, anayetumikia
nyongeza ya adhabu ya kufungiwa mechi moja zaidi kufuatia kutoa maneno makali
wakati akitolewa nje na mwamuzi walipocheza dhidi ya West Ham.
Mchezaji aliyechukua nafasi yake walipocheza dhidi ya Swansea
wiki iliyopita, Leonardo Ulloa, ataanza katika mchezo huo dhidi ya Man United
baada ya kupona maumivu ya mgongo.
MAONI
YA WACHAMBUZI
Guy Mowbray: "Nimetabiri kuwa katika mchezo huo
Man United itaifunga Leicester City'.
"Ndio, wanaweza kuongeza mwishoni mwa mchezo.
"Kitu ambacho hatutakuwa na wasiwasi nacho ni
kwamba Leicesterwatakuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya England, wakikumbushia
Arsenal mwaka 2002 kwa kuthibitisha hilo kwenye uwanja huo, ambayo umewahi
kuandaa sherehe nyingi za ubingwa mara nyingi kuliko mahali kwingine.
"Man United watataka kushinda mchezo huo kwenye
Uwanja wa Old Trafford, ili waweze kumaliza angalau katika nafasi ya nne za juu.”
"Mei Mosi mi alama ya kuanza vizuri, mwanzo mpya…”
WANACHOSEMA
MAKOCHA
Kocha wa Manchester United Louis van Gaal: "Nafikiri
tunatakiwa kuwafunga kwa sababu bado tuko katika mbio za kusaka nafasi ya nne.
Hatuwezi kukubali wawe mabingwa wikiendi hii kwenye uwanja wetu wa Old
Trafford.
"Nafikiri wanaweza kuwa mabingwa baadae wiki ijayo.
Hatuharibu sherehe yao, ila tunaiharisha tu kidogo.”
Kocha wa Leicester City Claudio Ranieri: "Ni kitu
kisichoaminika, ni historia na hilo tunalijua.
"Ni muhimu kumaliza historia
kama sinema ya Kimarekani. Wakati wote mwishoni ni mzuri, umalizika vizuri.
"Ni nafasi nzuri lakini kwa sababu hii tunatakiwa
kuangalia. Acha niw kimya, tusubiri, tuna muda bado.
"Niliwaambia, ‘kila
kitu kipo mikononi mwetu na lazima tuendelee’.
Watu wengine watafurahia hilo lakini mimi lazima kusonga mbele.”
UTABIRI WA LAWRO
Mchezo huu sio lazima Leicester ishindi lakini kwa Manchester
United, wanatakiwa kushinda kwa kuwa wanahitaji ushindi ili waendelee kubaki
katika nne bora.
Nafikiri mchezo huo utamalizika kwa sare, ambayo
itakuwa nzuri kwa Leicester, ingawa utachelewesha ubingwa wao hadi Jumatatu
usiku wakati Tottenham watakapocheza na Chelsea.
No comments:
Post a Comment