Timu ya soka ya Uchukuzi Sports Club ikifanya mazoezi wakijiandaa kwa mashindano ya Mei Mosi |
Na Cosmas Mlekani
TIMU ya Uchukuzi Sports
Club imetamba kufanya vizuri katika mashindano ya Mei Mosi yatakayofanyika
mjini Dodoma kuanzia Aprili 16 mwaka huu.
Wachezaji wa Uchukuzi Sports Club wakijifua kwa ajili ya Mei Mosi. |
Mwenyekiti wa timu
hiyo inayoundwa na wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Mohamed Ally alisema kuwa yake itafanya vizuri katika mashindano hayo.
Ally alisema kuwa
kwa sasa wako katika mazoezi makali kujiandaa na mashindano hayo, ambayo
yatafikia kilele chake Mei Mosi mjini Dodoma.
Akinana wa Uchukuzi wakijifua kwa ajili ya kuvuta kamba. |
Alisema Uchukuzi
Sports Club ina timu za soka, netiboli, kuvuta kamba, bao, karata, riadha,
baiskeli na vishale.
Alisema kuwa wana
uhakika timu yao kutamba katika mashindano hayo ya Mei Mosi kutokana na kufanya
maandalizi kabambe chini ya makocha wa kimataifa na wazoefu.
Ally aliwataja
baadhi ya makocha ho kuwa ni pamoja na Kenny Mwaisabula, Robert Damian, Terry,
Kingsley Malwilo na Abunu Issa, ambao wameifanya timu yao ya soka kuwa tishio
kwa timu zingine.
Alisema kuwa timu
zao hizo zimekuwa zikicheza mechi kibao za majaribio ili kuwawezesha makocha
kubaini makosa na kufanya marekebisho ya mwisho kabla timu hiyo haijaondoka
kwenda Dodoma.
Naye Meneja wa
Uchukuzi Sports Club, Damiani alisema kuwa timu yao inatarajia kwenda Dodoma
Aprili 14 tayari kwa mashindano hayo.
Alisema timu ya
soka na netiboli zimefanya majaribio kadhaa ili kujiweka fiti kwa mashindano
hayo, ambayo wana uhakika wa kutwaa ubingwa.
Kikosi kabambe cha timu ya soka ya Uchukuzi kikiwa pamoja na kocha na meneja wa timu hiyo Robert Damiani (kushoto). |
No comments:
Post a Comment