Baadhi ya wanariadha chipukizi wa Tanzania wakichuana katika moja ya mashindano kwenye Uwanja wa Taifa hivi karibuni. |
Na Mwandishi Wetu
RIADHA Tanzania (RT)
imetangaza majina 27 ya timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20
kwa ajili ya mashindano ya Afrika Mashariki na Kati yatakayofanyika nchini
Aprili 29 na 30.
Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa
timu hiyo Robert Kalyae, timu hiyo ya wanawake na wanaume ambayo itapiga kambi
katika shule za Filbert Bayi Mkuza Kibaha, imechaguliwa baada ya kufanyika mashindano
ya mchujo mara tatu.
Alisema kuwa mashindano
hayo ya mchujo yaliyofanyika Dar es Salaam, Mbeya na Arusha.
Timu ya wanaume inaundwa na
Adinani Haruna wa Moshi atakayeshiriki mbio za mita 100 na 200, Benjamin
Michael wa Dar es Salaam atakayeshiriki mbio za mita 100 na 200, Oscar Prosper
(Moshi) atakayekimbia mbio za mita 400.
Wengine ni Imani James na
John Silima wa Dar es Salaam watakimbia mbio za mita 400, Thobias Bula, Simon
Francis, Emmanuel Gadiye na Francis Dambel kutoka Karatu watakimbia mita 800 na
1500.
Wachezaji na viongozi wa timu ya mkoa wa Dar es Salaam katika picha ya pamoja baada ya kushiriki mashindano ya taifa mwaka jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. |
Kalyae aliwataja wachezaji
wengi wa timu hiyo kuwa ni pamoja na Elisha Wema wa Manyara na Jackson Makombe
wa Pwani mita 5,000.
Watakaorusha mkuki, kisahani
na tufe ni pamoja na Sabas Daniel wa Bagamoyo, kuruka chini ni Anthony Mwanga, anayesoma
Afrika Kusini, Dennis David wa Arusha, Hafidh Khalfan mita 400 na 800, na Jimmy
Kisumo wa shule ya sekondari Tambaza ya Dar es Salaam.
Kwa upande wa wanawake
waunaokimbia mbio za mita 100 na 200 ni Rehema John toka Magu, Jane Maiga wa
Pwani, (mita 400 na kuruka chini) watakuwa Hynes Bamopenja wa Dar es Salaam na
Rose Seif wa Pwani.
Watakokimbia mita 800 na
1500 ni pamoja na Dorcas Boniface, Regina Deogratius, Betrina Michael na Easter
Martin, Angelina Tsere mita 5,000 na Aisha Mohamed mita 5,000.
Mbali na Kalyae makocha
wengine watakaoinoa timu hiyo ni pamoja na Mwinga Mwanjala na Ephania Mugaza wakati
daktari ni Richard Yomba na meneja wa timu hiyo ni Peter Mwita.
Alisema vigezo walivyotumia
kuchagua timu hiyo ni pamoja na kuzingatia muda wa wachezaji katika mashindano
hayo ya majaribio, umri pamoja na bidii na kujituma.
can i have contacts of robert kalyae
ReplyDelete