LONDON, England
MCHEZAJI Zlatan Ibrahimovic anataka apewe kiasi cha pauni 600,000
(sawa na sh. 1,881,000,000)kwa wiki ili kuchezea klabu ya Ligi Kuu ya England.
Kiasi hicho cha fedha kimebainishwa na mchezaji huyo ambaye
ataondoka katika klabu yake ya sasa ya Paris Saint-Germain akiwa huru katika
kipindi cha majira ya joto.
'Tunataka kumsajili, lakini kiasi cha fedha anachotaka alipwe ndio
tatizo,' kilisema chanzo cha ndani. ‘Tukifanikiwa
hilo tutakuwa tumefanya jambo kubwa sana kumpata, lakini ukweli anahitaji kiasi
hicho cha fedha, akiwa na umri wa miaka 34?
Ibrahimovic amekuwa akifanya mazungumzo na timu za China, ambako
inasakiwa kuwa ameahidiwa kupewa kiasi cha pauni milioni 1 kwa wiki endapo
atatua huko, lakini hana mpango wa kuhamia Mashariki ya Mbali.
Badala yake ameziambia klabu za Uingereza kuongeza mshahara wake
aliokuwa akiupta PSG, ambako aliwapeleka mabingwa hao wa Ufaransa kutwaa taji
jingine.
Ibrahimovic yuko mbioni kwenda kucheza England lakini ikiwa na
maana kuwa kolabu moja itakuwa inatoa mshahara mkubwa nchini. Anaamini kuwa
hatakuwa na furaha kutokana na kodi zilizotozwa Uingereza.
Mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa katika Ligi Kuu ya England kwa
sasa ni Wayne Rooney, ambaye anaondoka na kitita cha pauni 260,000.
Arsenal, Manchester United, Chelsea na hata West Ham zimekuwa
zikihusishwa na mshambuliaji huyo wa Sweden.
Wakala wa Ibrahimovic Mino Raiola aliliambia gazeti la Dello
Sport: 'Ukiiondoa Manchester City, ambayo itamchukua (Pep) Guardiola, klabu
zote kubwa zimepiga hodi zikitaka kumchukua kocha huyo.
Mahitaji hayo makubwa anayotaka Ibrahimovic bila shaka
yatazigharimu klabu angalau pauni milioni 31 kwa msimu mmoja tu katika mkataba
wake huyo anaoutaka.
No comments:
Post a Comment