MADRID, Hispania
BARCELONA imevuliwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya
kufungwa mabao 2-0 na Atletico Madrid, zote za Hispania usiku wa kuamkia leo katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa
Vicente Calderon mjini Madrid.
Atletico Madrid wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada
ya awali kufungwa 2-1 Uwanja wa Camp Nou, Barcelona.
Mabao yote ya timu ya Muargentina Diego Simione leo yamefungwa na
Antoine Griezmann dakika ya 36 na lingine kwa penalti dakika ya 88.
Bayern
Munich imefakiwa kwa mbinde kwenda Nusu Fainali baada ya kuitoa Benfica kwa
ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya sare ya 2-2 leo Uwanja wa Luz.
Mabao ya Benfica yamefungwa na Raul Alonso Jimenez Rodriguez
dakika ya 27 na Anderson Souza Conceicao dakika ya 76, wakati ya Bayern
iliyoshnda 1-0 katika mchezo wa kwanza nyumbani wiki iliyopita, yamefungwa na
Arturo Vidal dakika ya 38 na Thomas Muller dakika ya 52.
Mshambuliaji Mfaransa wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann (aliyebebwa)
akishangilia bao pamoja na kiungo wa timu hiyo Gabi wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya juzi.
|
Atletico Madrid na Bayern Munich zinaungana na Real Madrid ya
Hispania na Manchester City ya England katika Nusu Fainali, ambayo droo yake
itapangwa Ijumaa.
Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro aliipeleka Real Madrid Nusu
Fainali juzi kwa mara ya sita mfululizo baada ya kufunga mabao matatu peke yake au hat-trick,
ikishinda 3-0 Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid dhidi ya Wolfsburg ya
Ujerumani.
Real imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya wiki
iliyopita kufungwa 2-0 Ujerumani na Ronaldo alifunga mabao yake katika dakika
za 15, 17 na 77 na kufikisha mabao 46 msimu huu kwenye mashindano yote.
Kevin de Bruyne naye alifunga bao pekee dakika ya 14 Uwanja wa
Etihad jana na kuipeleka Manchester Nusu Fainali kwa mara ya kwanza katika
historia yao kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya PSG.
Man City imesonga mbele kwa
ushindi wa jumla ya mabao 3-2 baada ya wiki iliyopita kulazimisha sare ya 2-2 mjini
Paris.
Ushindi huo unamfanta kocha Manuel Pellegrini kuweza kukutana na mrithi wake mwishoni
mwa msimu, Pep Guardiola baada ya Bayern Munich pia kuingia hatua hiyo ya Nusu Fainali.
No comments:
Post a Comment