LONDON, England
KIUNGO wa Manchester City Yaya Toure ataondoka katika klabu hiyo
mwishoni mwa msimu baada ya hadi sasa kutopewa mkataba mpya, amesema wakala
wake.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, ambaye ni mchezaji wa
kimataifa wa Ivory Coast, na ni mchezaji bora wa mwaka wa Afrika mara nne
mfululizo kuanzia mwaka 2011, alijiunga na klabu hiyo ya Ligi Kuu akitokea Barcelona
kwa pauni milioni 24 Julai mwaka 2010.
Miaka sita iliyopita Toure aliuzwa na aliyekuwa kocha wa Barca Pep
Guardiola, ambaye sasa anatua Man City kuchukua nafasi ya Manuel Pellegrini wakati
Mhispania huyo atakapoondoka Bayern Munich mwishoni mwa msimu.
"Tulisubiri kwa muda mrefu. Manchester City iliahidi kuongeza
mkataba lakini hakuna kilichofanyika hadi sasa, hivyo Yaya ataondoka Juni, “alisema wakala wake Dimitri Seluk.
"Bila shaka hilo litakuwa limesikitisha sana Yaya, lakini ni
mchezaji wa kulipwa atabaki katika mataba na ataendelea kuifanyia mazuri Man
City katika kipindi kilichobaki.”
Vyombo vya habari vimekuwa vikimuhusisha Toure na kutaka kuhamia Inter
Milan inayofundishwa na kocha wazamani wa Man City Roberto Mancini.
"Ofa kibao zimekuja zikitaka kumsajili Yaya na tunazichambua,
“alisema Seluk. "Inter? Tunazungumzia
kuhusu klabu kubwa.
"Kila mmoja anajua kuhusu uhusiano kati ya Yaya na Mancini lakini...bado
hatujafanya uamuzi wowote.
Toure alishinda taji la Ligi Kuu ya England akiwa na Man City
mwaka 2012 na 2014, Kombe la FA mwaka 2011 na lile la ligi mwaka 2014 na 2016.
Man City leo watakuwa wageni wa Paris St Germain katika mchezo wa
kwanza wa robo fainali wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.
No comments:
Post a Comment