Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp akimpongeza beki wake Alberto Moreno (katikati) wakati wa mchezo wa timu hiyo. |
LONDON, England
TIMU ya Borussia Dortmund kesho itashuka kwenye Uwanja wa Anfield kucheza
na wenyeji Liverpool katika mchezo wa marudiano wa robo fainali wa Ligi ya
Ulaya.
Bao la ugenini la Divock Origi, ambalo baadae lilifutwa na lile la kichwa la Mats Hummels na kufanya mchezo kuwa sare ya 1-1 mjini Dortmund, liliiweka Liverpool katika nafasi nzuri wakati Jurgen Klopp akirudiana na klabu yake yazamani.
Hatahivyo, kocha wa Dortmund Thomas Tuchel ana uhakika timu yake
inaweza kutinga nusu fainali licha ya Liverpool kuwa na rekodi nzuri dhidi ya
mpinzani wake huyo wa Ujerumani, ambapo Liverpool haijafungwa katika mechi 15.
"Pia tunaweza kufunga mabao ugenini, na tunaweza kufunga
zaidi ya bao moja, “alisema Tuchel,
ambaye timu yake imekata tamaa ya kuifukizia Bayern Munich katika Ligi Kuu ya
Ujerumani ya Bundesliga baada ya mara mbili kukubali kurudishwa mabao yake na
kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Schalke.
"Tulikuwa hauogopi. Tulipata nafasi kibao na kushinda, “alingeza, huku Dortmund ikiwa haijafungwa katika mechi 13 tangu
mwanzono mwa mwaka huu.
Kiungo wa Liverpool James Milner alisema kuwa watautumia vizuri
uwanja wao wa Anfield wakisaka kutwaa taji la 12 Ulaya, matatu yakitoka katika
michuano hii.
Ratiba
Kamili:
Shakhtar Donetsk v Braga
Matokeo mchezo wa kwanza: 2-1
Sparta Prague v Villarreal
Mchezo wa kwanza: 1-2
Sevilla v Athletic Bilbao
Mchezo wa kwanza: 2-1
Liverpool v Borussia Dortmund
Mchezo wa kwanza: 1-1
No comments:
Post a Comment