LONDON, England
UTEUZI wa Chelsea kumfanya Antonio Conte kuwa mbadala wa muda
mrefu wa Jose Mourinho hakuna maana yoyote, anasema mshambuliaji wazamani wa Blues
Chris Sutton.
Mourinho, 53, alitimuliwa Desemba nwaka jana akidaiwa kutoelewa na
baadhi ya wachezaji wakubwa wa timu hiyo.
Conte, alitua jijini hapa na kumwaga wino wa kuifundisha timu hiyo
kwa miaka mitatu baada ya kumalizika kwa msimu huu.
"Ikiwa atakuja hapa na kuanza kukorofishana na wachezaji,
basi anaweza kukosa mafanikio, “alisema Sutton.
Chini ya Mourinho, Chelsea ilitwaa taji la Ligi Kuu ya England
ikiwa na point inane zaidi msimu uliopita na pia ilitwaa Kombe la Ligi.
Lakini timu hiyo ilipoteza mechi zake tisa kati ya 16 za mwanzo za
ligi na walikuwa katika nafasi ya 16 katika msimamo, pointi moja juu ya ukanda
wa kushuka daraja, wakati Mourinho akitimuliwa.
Kocha wazamani wa Uholanzi Guus Hiddink, aliyeteuliwa kuchukua kwa
muda nafasi ya Mourinho hadi mwishoni mwa msimu, hajapoteza mchezo wowote kati
ya 15 tangu achukue timu hiyo.
Hatahivyo, the Blues imemchukua Conte, ambatye atawasili katika
klabu hiyo mara baada ya kumalizika kwa fainali za Mataifa ya Ulaya za Euro 2016 kama kocha wao wa kudumu.
"Chelsea walikuwa na nafasi nzuri ya kumbakisha Hiddink,"
aliongeza Sutton,mwenye umri wa miaka 43. “Na chini yake
timu iliimarika kila mahali.
Conte alishinda taji la Serie A katika miaka yake mitatu wakati
akiwa kocha wa Juventus, kabla hajaachia ngazi na kutua katika timu ya taifa ya
Italia mwaka 2014.
Wachezaji wazamani wa Chelsea Andy Townsend na Pat Nevin wote
wanaamini the Blues “imefanya
uteuzi mzuri”
.
"Sifikiri kama Conte atafanya tofauti na vile ambavyo alikuwa
akipenda Jose katika kiwango chake, “alisema
kiungo wazamani wa kimataifa wa Ireland Townsend.
Moja ya kazi ya Conte atakapotua Stamford Bridge inaweza kuwa ni
kufanya uamuzi wa mwisho kuhusu hatma ya John Terry.
Nahodha huyo wa Chelsea mwenye umri wa miaka 35 atamaliza mkataba
wake katika kipindi cha majira ya joto na anasema bado hajapewa mkataba mpya.
Lakini Townsend anaamini kuwa kuwasili kwa Conte kunaweza kusaidia
kuongeza mkataba kwa beki huyo wazamani wa England ili aweze kuendelea kubaki Stamford
Bridge.
Conte pamoja na kujihakikishia kibarua Chelsea, lakini hajaahidiwa
fungu na mmiliki wa timu hiyo Roman Abramovich ili kusajili wachezaji wapya.
Lakini mshambuliaji huyo wazamani wa England anafikiri the Blues itapambana
kuvutia wachezaji wa kubwa Ulaya bila kuvuruga sheria za matumizi ya fedha
katika usajili.
Chelsea,ambayo ilitwaa taji la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya mwaka
2012 na lile la Ligi ya Ulaya mwaka 2013, wako katika nafasi ya 10 katika Ligi
Kuu ya England, wakipitwa pointi 10 na timu nne za kwanza katika msimamo huo.
No comments:
Post a Comment