Kocha Rose Mkisi akihamasisha timu yake ya kuvuta kamba ya wanaume
ya TPDC walipocheza na Ukaguzi katika michuano ya Mei Mosi. TPDC walishinda kwa
mivuto 2-0.
|
Na Mwandishi Wetu
WACHEZAJI wa timu ya Uchukuzi SC inayoshiriki kwenye mashindano ya
Mei Mosi mkoani hapa, juzi wameibiwa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh
milioni 1.5 katika nyumba ya kulala wageni waliyofikia ya MT iliyopo Chadulu
mjini hapa.
Mkuu wa Upelelezi wa wilaya, Charles Chalula, alipoulizwa juu ya
tukio hilo jana alikiri taarifa kufika ofisini kwake, na tayari jeshi hilo
linawashikilia watu watatu akiwemo mhudumu wa hoteli hiyo.
Pia alisema
atawasiliana na mkurugenzi wa hoteli hiyo, aliyemtaja kwa jina moja la Haule
ili aweze kurudisha fedha za wachezaji, ambazo walilipa kukaa hapo hadi Mei 2
mwaka huu michezo itakapokamilika.
"Ni kweli wachezaji wamekuwa na hofu na usalama wao na mali zao,
nitamtafuta mmiliki wake akiwezekana arudishe fedha zao leo hii hii (jana) ili waweze
kuhamia hoteli nyingine, ila nitahakikisha suala la upelelezi tunalifanya
haraka ili hivi vitu vilivyoibwa vipatikane haraka,” alisema Chalula.
Timu ya kamba ya wanaume ya Ukaguzi wakivutana na wenzao wa TPDC,
lakini walishindwa kwa mivuto 2-0.
|
Mbali ya soka, wachezaji wengine wa Uchukuzi ni wa michezo ya kuvuta
kamba, bao, drafti na karata. Mmoja wa wachezaji hao, Ally Suleiman katika
chumba chake ameibiwa kompyuta mpakato yenye thamani ya Sh milioni 1.2, fedha
taslimu Sh 120,000 na mashine inayohifadhia nyaraka mbalimbali yenye thamani ya
Sh 180,000.
Thea Samjela wa Uchukuzi SC (kuilia) akichuana na Regina Mutimangi
wa TPDC katika mchezo wa bao.
|
Aliongeza kuwa, walifungua chumba cha mchezaji mwingine, Aminiel Ombeni ambaye
amesafiri kwenda Moshi kuzika baada ya kupata msiba wa mama yake, na bado
haijajulikana vilivyoibwa kwani begi lake lilikutwa katika chumba cha mteja aliyefika juzi mchana.
Naye
Katibu Mkuu wa timu ya Uchukuzi, Alex Temba alisema wamesikitishwa na tukio
hilo kwani haijawahi kutokea katika mikoa yote waliyowahi kushiriki michezo ya
Mei Mosi.
Neema Makassy wa Uchukuzi
SC (kulia) akitafakari katika mchezo wa bao dhidi ya Joyce Kimondi wa Ujenzi.
|
"Suala hili limetusikitisha sana
huyu ni mfanyakazi mwenzetu pamoja na kwamba tupo katika suala la michezo
lakini aliendelea na kazi za ofisi na jana tu alikuwa akituma taarifa
mbalimbali, basi tunawaomba polisi watusaidie hivi vitu vipatikane, na hata
waongeze ulinzi kwani ni tukio la aibu kuwaibia wageni,” alisema Temba.
No comments:
Post a Comment