1. Mlango wa kuingilia abiria kwenye Kiwanja
cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), wanaotoka nje ya nchi, ambao
baadhi ya ndege zimelengwa kutokana na abiria wake aidha kupita au kuanzia
safari kwenye nchi ya Kongo iliyotangazwa kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola.
Na Mwandishi Wetu
KITENGO cha Afya katika Kiwanja cha
Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kimeweka udhibiti madhubuti
wa kujikinga na usambazaji wa magonjwa ambukizi, ikiwemo Ebola.
Ugonjwa wa Ebola unaosambazwa kwa virusi
vya Ebola, husababisha homa kali inayoweza kuambatana na kutokwa damu mdomoni,
puani, masikioni, machoni na sehemu nyingine za wazi na unaenea kwa haraka.
Hivi karibuni umetangazwa kutokea nchini
Kongo na kusababisha vifo.
Akizungumzia kuhusiana na mikakati hiyo
ya kupambana na magonjwa ambukizi ukiwemo wa Ebola, Ofisa Afya Mfawidhi
wa JNIA, Dk. George Ndaki alisema wanatoa mafunzo kwa watumishi na wahusika
wote wanaotumia kiwanja hicho katika kujikinga na magonjwa hayo.
“Sisi tumejiandaa vizuri na
tumeshafanya jitihada zote tumeshatoa maelekezo, mafunzo na kamati mbalimbali
za kiwanja zimejipanga kudhibiti magonjwa yote ya kuambukiza, ikiwemo sisi
wenyewe kujikinga na kuwakinga na abiria wote wanaotoka katika nchi hatarishi”,
alisema Dkt. Ndaki.
Aidha, akizungumzia kuhusiana na
utaratibu ambao Kiwanja kimeweka ili kuhakikisha abiria wenye maambukizi
wanapokelewa kwa tahadhari, ambapo wanapowasili na ndege zinazotoka nje ya nchi
zinazopakia abiria wanaosafiri kutoka katika nchi zinazoshirikiana na Kongo
hutakiwa kusafisha mikono kwa dawa maalum mara waingiapo katika eneo la
kuwasili.
1.
Mmoja wa abiria aliyewasili na ndege ya
Rwanda Air kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA),
akinawa mikono kwa dawa maalum inayoua vijidudu vya maradhi mbalimbali
yanayoambukiza, ukiwemo Ebola uliotangazwa hivi karibuni umeibuka nchini Kongo.
“Abiria wote wanapowasili hupita katika
eneo maalum ambalo wote hutakiwa kuosha mikono, lakini pia kuna mashine ambazo
zimewekwa ili kuweza kuwatambua abiria ambao wanawasili wakiwa na hali ya joto
isiyokuwa ya kawaida mfano kuwa na joto la juu sana kuanzia 38oC,
ukiachana na hilo kuna fomu maalum ambazo abiria wanapowasili hujaza na pia
taarifa kutoka kwa rubani wa ndege kama kuna abiria ana maambukizi kwenye
ndege. Baada ya kumtambua mgonjwa basi atapitishwa katika njia ya tofauti na
abiria wengine na kupakiwa katika gari la wagonjwa na kupelekwa Temeke
Hospital,” alisema Dk. Ndaki.
1. Ofisa Afya Mfawidhi wa Kiwanja cha
Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Dkt. George Ndaki akionesha
mashine maalum inayompima abiria (thermo scanners) mara anapopita eneo la
ukaguzi wa afya, ambapo linakuwa likisomwa na Afisa Afya kwenye komputa iliyopo
(kulia). JNIA wamejidhatiti na makonjwa ya milipuko ukiwemo wa ebola
uliotangazwa kuwepo nchini Kongo.
“Kwanza kabisa kwa abiria wote ambao
wanatokea katika nchi ambazo zinasadikika kuwa na maambukizi wanapowasili
wanakuwa sanitized (wanaosha mikono na dawa maalum) ili wasiweze kuleta
maambukizi ndani, lakini pia tuna thermo scanners (mashine ambazo
zinaangalia hali ya joto la mtu) anapowasili ambapo tunapogundua mgonjwa
anamatatizo tunapeleka isolation (Chumba cha wagonjwa wa kipekee) na baada ya
hapo anapelekwa katika vyumba vya waonjwa waliotengwa katika hospitali ya
Temeke” alibainisha Bw. Rwegasha.
1.
Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Paul Rwegasha (kulia) akizungumza na
waandishi wa habari juu ya udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kwenye kiwanja
hicho. Hivi karibuni ugonjwa wa Ebola umetangazwa kutokea nchini Kongo.
Katika hatua nyingine Dk. Ndaki alisema
mpaka sasa hakuna mgonjwa yeyote ambaye amebainika kuwa na ugonjwa wa Ebola
kupitia JNIA.
Dk Ndaki ametaja namna ya kujikinga na
ugonjwa wa Ebola ni pamoja na kuepuka kugusa damu, machozi, jasho, matapishi,
kamasi, mkojo au kinyesi cha mtu mwenye dalili za ugonjwa; pia mtu hatakiwi
kugusa, kuosha au kuzika maiti ya aliyekufa kwa Ebola; pia usiguse au kula
wanyama kama popo, sokwe au swala wa msituni.
Dalili za Ebola ni pamoja na homa kali,
maumivu ya kichwa na misuli, mwili kulegea, kutapika, kuharisha, vipele ma
kutokwa damu
“Natoa wito tu kwa wananchi kuhakikisha
wanafuata taratibu zote tulizoziweka ili kuhakikisha kwamba hatupati mgonjwa
yeyote katika nchi yetu. Kama kila mtu atatekeleza wajibu wake kwa abiria kufuata
taratibu, wanaosimamia masuala ya afya wakitimiza wajibu wao, na Kiwanja
kikitimiza wajibu wake basi hakika magonjwa ya mlipuko
hayataweza kufika katika nchi yetu” alieleza Dkt. Ndaki.
No comments:
Post a Comment