LONDON,
England
RAFAEL Benitez amesisitiza kuwa hajutii kumruhusu
mshambuliaji, Aleksandar Mitrovic kuondoka kwenye klabu ya Newcastle United na kutua Fulham.
Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Serbia mwenye umri wa miaka 23, alijiunga na Fulham kwa
ada ya uhamisho ya pauni milioni 27, amefunga mabao sita kwenye mechi tano
zilizopita kwenye klabu yake na timu ya taifa, yakiwemo mabao manne kwenye Ligi
Kuu ya England.
Kinyume chake, Newcastle imefunga mabao matatu kwenye mechi zake
nne za Ligi Kuu ya England, huku kocha Benitez akiziba pengo la mshambuliaji
huyo kwa kumleta mshambuliaji Salomon Rondon kwa mkopo wa muda mrefu kutoka
West Brom, huku Dwight Gayle akienda upande mwingine na Benitez akimsajili
Yoshinori Muto kutoka Mainz kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 9.5.
Kuuzwa kwa Mitrovic
kumeibua maswali kwa mashabiki wa Newcastle, lakini Benitez haonekani kujutia hilo.
Alipoulizwa kiwango cha
Mitrovic msimu huu Benitez alijibu: "Anafanya vizuri, alifanya
vizuri na Serbia, lakini Rondon anafanya vizuri na Venezuela.
"Kila mchezaji ana mazingira yake na anaweza akafanya vizuri
kwenye timu moja lakini hasifanye vizuri timu nyingine.
"Tunatakiwa kufanya maamuzi kwa kuangalia kinachohitajika na
tulijua nini tunahitaji, hiko hivyo, sasa tunatakiwa kusonga mbele.
"Haitabadili uamuzi wangu. Natakiwa kusonga mbele na Ayoze
Perez, Joselu, Yoshinori Mutuo na Rondon, hiko hivyo."
No comments:
Post a Comment