Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela
(kushoto) akimkabidhi moja kati ya fulana 100, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya
Taifa, Prof. Audax Mabula (kulia), zilizotolewa na TAA kwa ajili ya Tamasha la
Urithi Wetu kwa mkoa wa Dar es Salaam litakaloanza Oktoba Mosi, 2018, katika Kijiji cha Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), katika
kuunga mkono Tamasha la Urithi Wetu, imekabidhi fulana 100 katika hafla
iliyofanyika Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Richard Mayongela alisema leo kuwa, wanaunga mkono tamasha hilo kwani linatangaza utalii wa nchini na alikabidhi fulana hizo kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Makumbusho ya Taifa, Professor Audax Mabula katika hafla hiyo
jijini Dar es Salaam.
Tamasha hilo
ambalo lilizindulia mjini Dodoma mwezi huu, litafanyika jijini Dar es Salaam
Oktoba Mosi katika Makumbusho ya Taifa, ambapo watu kibao wanatarajia
kuhudhuria kabla ya kufanyika Zanzibar na baadae mikoa mingine.
Pia TAA imetangazwa kuwa mshirika wa tamasha hilo kwa
ajili ya kutangaza utalii wan chi hiyo, ambapo mamlaka hiyo imeahidi kutangaza
tamasha hilo katika viwanja vyake nchini.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela
(katikati), Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof. Audax Mabula (kulia) na
Mratibu wa Tamasha la Urithi Wetu Dk. Emannuel Bwasiri (kushoto) kwa pamoja wakionesha
aina tatu za tisheti kati ya 100 zilizotolewa na TAA, kwa ajili ya Tamasha la
Urithi Wetu kwa mkoa wa Dar es Salaam, katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini
Dar es Salaam.
Mayongela aliongeza kusema kuwa wameamua kujihusisha
na tamasha hilo kwa kuwa viwanja vya ndege ni njia kubwa ya watalii kungia
nchini, hivyo ni muhimu kujihusisha na tamasha hilo, ambalo lilizinduliwa
na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.
“Kama mchango wetu katika tamasha hili, TAA inawapa
waandaaji wa Tamasha la Urithi nafasi ya kujitangaza katika viwanja vyetu vyote
vya ndege ili kusaidia kuutagaza utalii na kufanikisha kuingia kwa watalii
nchini, “alisema Mayongela.
Tamasha hilo ambalo litakuwa likifanyika kila mwaka,
linaandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, ambalo lilizinduliwa rasmi
Septemba 15 mjini Dodoma na likiwa na lengo la kuongeza idadi ya watalii nchini
kutoka milioni 1.3 mwaka jana ma kuongezeka zaidi.
Aidha, marais watatu wazamani wa Tanzania ni miongoni
mwa watu walioalikwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kuhudhuria tamasha hilo
la Oktoba Mosi.
Baada ya Dar es Salaam, Prtofesa Mabula alisema kuwa
tamasha hilo litatua Jijini Arusha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri
Abeid na Karatu, ambako ni njia
kuu ya kuingilia katika Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro na Serengeti kuanzia
Oktoba 8 hadi 13
No comments:
Post a Comment