Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) Bw. Richard Mayongela akimpa pole mjane wa Marehemu Bw. Charles Salim nyumbani kwake Chang’ombe jijini
Dar es Salaam.
|
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela leo meongoza mamia ya Wafanyakazi wa Mamlaka
hiyo kuuaga mwili wa Ofisa Usalama Mwandamizi wa Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), aliyefarikijuzi Tarehe 6/9/2018 katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kupatwa na
shambulio la moyo.
Akisoma wasifu wa marehemu, Bw. Mayongela amesema
Mamlaka itaendelea kushirikiana na familia ya marehemu, ambaye ameacha mjane na
watoto wawili.
“TAA kama mwajiri wa marehemu tumefanikisha shughuli
zote za hapa msibani natupo tayari kushirikiana na familia ya marehemi hata
baada ya msiba huu kumalizika, "alisema Mayongela.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Bw. Richard Mayongela akitoa salamu za rambimbi katika msiba wa Bw Charles Salim Chang'ombe Jijini Dar es Salaam. |
Naye msemaji wa Familia, Bw. Herbert Semwaiko aliishukuru
TAA kwa ushirikiano walionesha tangu kuugua ghafla kwa marehemu hadi kufariki
kwake.
“Sina maneno zaidi ya kusema pamoja na Kiswahili ni lugha
pana zaidi, ila nasema asante sana tunawashukuru kwa ushirikianowenu
mliouonesha, ambapo mmetusaidia kuanzia mwanzo wa ugonjwa wa ghafla hadi
kufariki kwake kijana wetu, Charles, "anasema Bw. Semwaiko.
Kwa upande wake, Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la
Anglikana, Daniel Mhando katika ibada yake fupi ya kumuombea marehemu aliwataka
waombolezaji kumuombea katikasafari ya mwisho atazikkwa Jumapili Septemba 9,
2018 wilayani Muheza mkoani Tanga.
Marehemu alizaliwa tarehe Oktoba 3, 1963 na kupata
elimu yake ya msingi katika shule ya Kibasila Jijini Dar es Salaam na baadae
elimu ya sekondari katika shule ya Hengongo mkoani Tanga, ambapo alihitimu
kidato cha nne mwaka 1983 na mwaka 1984 aliajiriwa serikalini na kupangiwa kazi
Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Dar es Salaam, kama Ofisa Usalama, na mwaka
2015 alipandishwa cheo na kuwa Ofisa Usalama Mwandamizi.
Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa Jina Lake Lihimidiwe. Amina.
Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa Jina Lake Lihimidiwe. Amina.
No comments:
Post a Comment