MONACO, Ufaransa
TIMU ya Atletico Madrid ilitoka nyuma na kuifunga Monaco
2-1 katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi A wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya
uliofanyika hapa.
Wenyeji Monaco ndio walikuwa wa kwanza kupata bao la
kongoza kupitia kwa Samuel Grandsir baada ya kutumia vizuri makosa ya uzuiaji
yaliyofanywa na wote, Saul na Angel Correa.
Diego Costa aliisawazishia Atletico Madrid baada ya
kupata pasi safi kutoka kwa Antoine Griezmann na kufunga bao huku Jose Gimenez akifunga
kwa kichwa kocha ya Koke na kuwapatia wageni uongozi wa mchezo huo.
Lakini Atletico, huku kocha wake Diego Simeone akiwa
jukwaani, nusura wafungwe bao katika dakika za majeruhi wakati mpira wa kichwa
uliopigwa na Kamil Glik ulipopaa juu ya lango.
Kocha huyo Muargentina alikuwa akitumikia mechi yake
ya mwisho baada ya kufungiwa mechi nne za Ulaya, baada ya kufanya kosa katika
mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Ulaya walipocheza dhidi ya Arsenal.
Winga Thomas Lemar, aliyesajiliwa kwa pauni Milioni 62
akitokea Monaco, alipata mapokezi mazuri wakati alipoingia katika kipindi cha
pili akiichezea Atletico.
Wachezaji wa Monaco. |
Katika Kundi C, mashabiki 50,.000 walishuhudia timu
ya Red Star Belgrade ikitoka suluhu na kikosi cha kocha wa Napoli, Carlo
Ancelotti katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya tangu mwaka 1992.
Katika mchezo mwingine, kipa wa FC Porto Iker
Casillas amekuwa mchezaji wa kwanza katika kampeni tofauti 20 za Ligi ya
Mabingwa wa Ulaya baada ya timu yake kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Schalke katika
mchezo wa Kundi D, huku Galatasaray ikiifunga Lokomotiv Moscow 3-0.
No comments:
Post a Comment