1.
Wachezaji
wa timu ya wanawake na wanaume ya kuvuta Kamba ya Klabu ya Uchukuzi (USC)
wakifanya mazoezi jana nyuma ya jengo la Aviation Banana ya kujiandaa na mashindano
ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara za Serikali na Ofisi za Wakuu wa
Mikoa (SHIMIWI), iliyopangwa kuanza Septemba 25 mkoani Dodoma.
Na
Mwandishi Wetu
KLABU
ya michezo ya Uchukuzi (USC), imeanza kujifua kwa ajili ya kushiriki Mashindano
ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara za Serikali zinazojitegemea, Wakala
wa Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (Shimiwi), itakayoanza Septemba 25
kwenye viwanja mbalimbali mkoani Dodoma.
Kwa
mujibu wa Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Mbura Tenga amesema wameanza kujifua kwa
nguvu ili kurudi na ubingwa wa michezo mbalimbali waliyoshinda kwa mara ya
mwisho michezo hiyo ilipofanyika mwaka 2014.
Tenga
amesema USC watashiriki kwenye michezo tisa, ambayo imeandaliwa na Shimiwi,
ambayo ni mpira wa miguu, netiboli, kuvuta Kamba, riadha, bao, karata, draft,
baiskeli na Darts.
“Tunauhakika
wa kwenda kufanya vizuri kwani timu imeanza mazoezi tayari ingawa muda ni
mdogo, ila ninaamini tutafanya vizuri,” amesema Tenga.
USC
inatetea vikombe vinne walivyoshinda mwaka 2014, ambavyo
ni Darts – wanaume (washindi wa kwanza); mpira wa miguu (washindi wa pili); na
Kamba – wanaume na baiskeli - wanawake (washindi wa tatu).
Ratiba
iliyotolewa na Shimiwi inaonesha katika ufunguzi mabingwa watetezi katika
mchezo wa kuvuta Kamba wanaume timu ya Ofisi ya Rais Ikulu itavutana na MSD;
nao wanawake wa RAS Iringa ambao ni mabingwa watetezi watavutana na Viwanda;
huku katika mpira wa miguu Wizara ya Elimu watakutana na Ukaguzi.
Michezo
hiyo ambayo pamoja na kuunganisha wafanyakazi wa umma wa maeneo mbalimbali pia
huleta burudani kwa wakazi wa eneo husika.
No comments:
Post a Comment