Monday, 10 September 2018

Aliyemfunga Serena Williams Apigiwa Debe


NEW YORK, Marekani
BINGWA mpya wa mashindano ya tenisi ya US Open, Naomi Osaka (pichani) anaweza kuwa Mjapan wa kwanza kuwa katika nafasi ya namba moja duniani, anasewma mchezaji wazamani wa mashindano makubwa aliyewahi kutinga nusu fainali, Kimiko Date.

Osaka, mwenye umri wa miaka 20, alishinda seti mfululizo Jumamosi wakati akitwaa taji la US Open kwa wanawake, lakini ushindi wake huo ulifunikwa na kelele za Serena Williams dhidi ya waamuzi.

Lakini, Date alisema ushindi wa kwanza wa Osaka katika fainali ya mashindano makubwa ni wa aina yake.

"Ikiwa ataendelea kufanya kama alivyofanya katika wiki mbili za nyuma, hakuna shaka ataendelea na kuwa Mjapan wa kwanza kuwa katika namba moja dunia katika ubora wa mchezo huo, “aliongeza Date.
Naomi Osaka.
Osaka – ambaye alizaliwa Japan na alikulia Marekani, amepanda katika viwango baada ya ushindi huo jijini hapa hadi kufikia nafasi ya saba kwa ubora duniani.

Date, ambaye ni mchezaji aliyefikia nusu fainali ya mashindano ya Wimbledon mwaka 1996, anatarajia Osaka ataendeleza mafanikio ya Mchina, Li Na, ambaye ni bingwa mara mbili wa mashindano makubwa.

Date ambaye ni bingwa namba nne wazamani duniani alisema: “"Osaka ameingia katika nguvu ya tenisi ya wanawake kwa nguvu zake mwenyewe kama mchezaji wa Asia, mchezaji Mjapan.

"Hadi sasa Li Na pekee (mchezaji wa Asia) yuko fiti kukabiliana na aina ile ya nguvu.
"Unaweza kumwambia Serena alikuwa akihofia nguvu ya Osaka.”
Serena Williams.
Williams aliwabwatukia waamuzi baada ya mchezo huo, yuko matatani baada ya kuwaambia waamuzi kuwa ni “wezi” na “waongo”.

No comments:

Post a Comment