BARCELONA, Hispania
KIUNGO wa kimataifa wa Croatia, Ivan Rakitic amekuwa akihusishwa
na kujiunga na klabu ya Paris Saint-Germain (PSG), lakini amesema hakuna
anayeweza kumuondoa Barcelona.
Rakitic haoni hatma yake nje ya Barcelona pamoja na kuwindwa na
klabu ya PSG.
PSG wamekuwa wakimuwania kiungo huyo wa kimataifa wa Croatia, ambaye
aling’ara na timu yake ya taifa kwenye fainali za Kombe la Dunia, lakini Rakitic aliweka wazi kuwa hana mpango
wa kuondoka Barcelona.
Rakitic, ambaye alishinda La Liga na mataji matatu ya Ulaya
katika msimu wake wa kwanza akiwa na Barcelona mwaka 2015, alitoa mchango
mkubwa kwenye kikosi cha kocha Ernest Vervede kushinda taji la La Liga msimu
uliopita, anatazamiwa kuwa nahodha ajaye wa timu hiyo kufuatia kuondoka kwa
kiungo Andres Iniesta na Javier Mascherano.
"Sioni pakwenda nikiondoka,” alisema Rakitic. “Kuna mada
mbalimbali tumezungumza. Nilichukua siku kadhaa kufikiria na kugundua nilipo.
“Sioni kitu chochote
maalumu, najiona nina bahati. Naweza kucheza Barcelona, kuipigania beji hii na
hicho kitu kikubwa. Pia mke wangu na mtoto wangu wa kike wanafuraha Barcelona.”
Rakitic ameanza kwenye
mechi zote tatu za La Liga, ambazo Barcelona imeshinda msimu huu na kuiwezesha
klabu hiyo kuongoza katika msimamo wa
Ligi Kuu ya Hispania, La Liga.
No comments:
Post a Comment