Na
Mwandishi Wetu
IKIWA
zimepita siku kadhaa tangu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kutoa
ufafanuzi juu ya tuhuma za wizi katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha
Julius Nyerere (JNIA), Mtanzania aishie nje ya nchi amejitokeza na kuipongeza
TAA kwa ubora wa huduma ambazo inatoa kwa watumiaji wa uwanja huo.
Mtanzania
huyo aliyefahamika kwa jina la Bw. Barnabas Kijika ameipongeza TAA kwa taarifa
nzuri ambayo imeitoa kwa Umma kuhusiana na suala la kupotelewa mizigo kwakuwa
hata yeye alishawahi kupotelewa mizigo JNIA lakini alipofuatilia alipata yote
ikiwa haijaibiwa.
“Mimi
nasikia moyo wa kuishukuru TAA na wafanyakazi wote kwa sababu hata mimi hili
suala hilo limewahi kunitokea kipindi nimekuja Tanzania nikitokea nchi za
Uarabuni ambapo mizigo miwili ikawa imepotea.
Lakini
nikatoa maelezo kwa wahusika na baada ya siku moja nikapigiwa simu kupitia
namba niliyoacha kwa ajili ya kupewa taarifa kwamba mizigo yangu imepatikana na
nilipoikagua nikakuta mizigo yangu ipo salama yote hakuna kilichopotea,”
amesema Bw. Kijika.
Pia
Bw. Kijika amesema siku za nyuma alishughudia baada ya siku moja upatikanaji wa
mizigo ya watalii wawili waliokuwa wakisafiri kupitia JNIA baada ya taarifa ya
kupotea kwa mizigo hiyo kuwafikia wafanyakazi wa JNIA.
Katika
sehemu ya barua pepe ambayo Bw. Kijika alituma kupitia anwani ya info@airports.go.tz
na sauti aliyojirekodi na kuirusha kwa njia ya Whatsapp amebainisha kwamba, kwa
muda mrefu amekuwa akitumia viwanja mbalimbali vya ndege vya Tanzania na
changamoto ambazo anaziona ni za kawaida.
“Kwa
zaidi ya miaka 15 nimekuwa nikitumia airports za Tanzania sijawahi kujuta
isipokuwa changamoto za kawaida hata Ulaya zipo,” amebainisha Bw. Kijika.
Hivi
karibuni abiria mmoja Mtanzania mwenye asili ya Kiarabu alilalamikia kuibiwa
pochi lenye fedha na vitambulisho mbalimbali wakati akisafiri kupitia JNIA
kwenda nchi za Falme za Kiarabu, ambapo hata hivyo Kaka yake, Bw. Wael Hassan
alipooneshwa picha zilizopigwa na kamera za usalama (CCTV), walikiri hakuna
uwizi wowote na ndugu yao hakuibiwa na aliomba radhi kwa niaba ya ndugu yao
huyo.
No comments:
Post a Comment