1. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), Bw. Richard Mayongela (katikati) jana akijadili jambo na Kaimu
Mkurugenzi wa Fedha na Biashara, Bw. Pius Wankali (kulia) na Kaimu Meneja Mipango na Takwimu, Bw. Nasib Elias (mwenye fulana ya bluu bahari) kabla
ya mkutano na Wendeshaji wa Mashirika ya ndege kuanza kwenye ukumbi wa Jengo la
Pili la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Myerere (JNIA-TB2).
Kushoto ni Kaimu Mwanasheria wa TAA, Bw. Elius Mwashiuya.
Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), jana imewataarifu Waendeshaji wa Mashirika
ya ndege za abiria zinazofanya safari zake kuanzia kwenye Kiwanja cha Ndege
cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) juu ya tozo mpya ya Huduma za Viwanja vya Ndege.
Mkurugenzi
Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela amewaeleza kuwa utekelezaji wa tozo hiyo, ambayo
ni dola tano (5) kwa abiria wa nje ya nchi na abiria wa ndani ni Sh. 5,000, utaanza
rasmi Oktoba 1, 2018.
Bw.
Mayongela amesema lengo la tozo hiyo ni uboreshwaji wa huduma na
miundombinu ya Usalama katika Viwanja vya Ndege nchini ili kuhakikisha vinafikia
viwango vya ubora vya Kimataifa na pia kutoa huduma bora za kiusalama kwa wadau
wake.
Akitoa
ufafanuzi zaidi kuhusiana na ada hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Biashara wa
TAA, Bw. Pius Wankali ameeleza kwamba agizo la ukusanywaji wa tozo hiyo
ulitangazwa rasmi na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) mwezi Juni mwaka
huu.
“Tangazo
la kuanzishwa kwa tozo hii lilichapishwa na TCAA kutoka kwenye nyaraka AIC Doc
No. TCAA/FRM/ANS/AIS-30, tarehe 29 Juni, 2018 na utekelezaji wake utakuwa ni
kuanzia Oktoba Mosi, 2018," amesema Bw. Wankali.
Kwa
upande wa wawakilishi wa mashirika ya ndege kubwa kutoka Shirika la ndege
Tanzania (ATCL), Bw. Ismail Ismail alitaka kuwepo kwa maelezo ya kina juu ya
tozo hiyo, ambayo alitaka ijumuishwe ndani ya tiketi ili abiria awe ameilipia
moja kwa moja.
1. Waendeshaji wa Mashirika ya Ndege zinazofanya safari zake kwa
kuanzia kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA),
wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),
Bw. Richard Mayongela (katikati mbele) jana alipozungumza nao kuhusiana na tozo
ya Huduma ya Viwanja vya Ndege, ambayo itaanza rasmi kutumika Oktoba 1, 2018.
Mwenyekiti
wa Waendeshaji wa Ndege ndogo za abiria, Chief Uyeka Rumbyambya amesema kuwe na
taratibu za kumuhusisha Mkurugenzi Mkuu katika mikutano mbalimbali ya
Waendeshaji wa Mashirika ya ndege, ili waweze kuwasilisha.
1. Naye
Kaimu Meneja Mipango na Takwimu wa TAA, ambaye ni mratibu wa mkutano huo,
Bw. Nasib Elias alitoa ufafanuzi juu ya ukusanywaji wa tozo hii, ambayo
inatarajiwa pia kuwa ni moja ya chanzo cha mapato cha Mamlaka.
1. Mwenyekiti
wa Waendeshaji wa mashirika ya ndege ndogo za abiria, Chief Uyeka Rumbyambya
akitoa mapendekezo kwa ajili ya maboresho wakati wa kikao kati ya uongozi wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na waendeshaji hao uliofanyika jana
kwenye Jengo la Pili la abiria la Julius Nyerere (JNIA-TB II).
No comments:
Post a Comment