Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imesisisitiza kuwa wananchi wa Kipunguni A
na Kipunguni Mashariki, ambao wanatakiwa kuondoka katika maeneo hayo ili kupisha
upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), watapatiwa
viwanja mahali pengine pamoja na kulipwa fedha, imesisitizwa.
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye alipozungumza na baadhi ya wakazi wa
maeneo hayo katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa JNIA Terminal I kuhusu upanuzi wa kiwanja hicho.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela wakati Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye alipozungumza na wakazi wa Kipunguni. |
Alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John
Pombe Magufuli kamwe haina nia ya kuwaumiza wananchi, ambapo watu wenye nyumba
maeneo hayo watapatiwa viwanja katika maeneo ya Msongola na kupewa fidia ya
fedha.
Alisema kuwa siku zote Serikali ya Magufuli inataka kuhakikisha
kila mwananchi anapata haki yake anayostahili na sio kumuumiza.
Alisema kuwa jumla ya wananchi 801 walitakiwa kupewa
viwanja na tayari Kampuni ya Tanzania Remix ilishaandaa viwanja 537 kwa ajili
ya awamu ya kwanza ya ugawaji viwanja hivyo.
Zoezi hilo kwa miaka mingi lilishindwa kufanyika
licha ya Serikali kufanya tathmini, na sasa litafanikiwa baada ya wananchi
kurudhika na maelezo ya Nditiye baada ya kusema kuwa hata wale ambao
hawakufanyiwa tahmini wakati ule, alimuagiza Naibu Mkurugenzi Mkuu kuhakikisha
wanafanyiwa tathmini ili nao wapatiwe viwanja na fedha wanazostahili.
Alisema tathmini ya awali ilifanyika mwaka 2013 na
kusema kuwa wale watakaovunjiwa nyumba zao watapatiwa viwanja na watafidiwa
fedha.
Aidha, Naibu waziri alisema wote waliopewa viwanja
baada ya kuvunjiwa Kigilagila, ambao hawakuwa wakazi wa eneo hilo na Kipawa,
watanyang’anywa viwanja hivyo na kuchukulia hatua za kisheria.
Alisema hata kama watakuwa wamejnga nyuma, lakini
wakabainika kuwa walipewa viwanja wakati hawakuwa wakazi wa maeneo hayo,
watapokonywa mara moja na kuchukuliwa hatua.
Alisema kuwa baada ya tahthmini kufanyika muda mrefu,
wananchi hao wataongezewa asimilia ya fedha za awali kulingana na miaka iliyopo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Richard Mayongela
alisema kuwa maelekezo yaliyolewa na Naibu waziri atayafanyia kazi na ataunda
tume kama alivyoagizwa ili kuhakikisha utekezaji unafanyika kwa ufanisi.
Mayongela alisema kuwa yeye kama mtendaji
atahakikisha matatizo yote yaliyojitokexa na tayari mchakato wa kushughulikia
tatizo hilo ulianza muda mrefu na ameanza kufanikiwa.
Alimtaka Mbunge wa Segerea, Mona Karia kumuagiza
kaimu mkurugenzi huyo mkuu wa TAA kazi yoyote nay eye yuko tayari kuitekeleza
ili kuhakikisha wanamaliza matatizo yote.
Alisema tayari viwanja 537 vyenye thamani ya Sh
bilioni 3.7 vilishakbidhiwa kwa TAA mwezi uliopita pamoja na kuchelewa, lakini wameshapata viwanja 700 lakini
wanatakiwa kwenda kuvihakiki kama kweli vipo kwa ajili ya kuwapatia wahusika.
Alisema kuwa
tayari wananchi 57 kati ya 59 walishabomoa nujmba zao hadi mwezi uliopita na
wamebaki wawili,ambao anategemea nao wakati wowote watavunja nyumba zao na
kuondoka eneo hilo.
Alisema wiki hii ataunda kikosi kazi ambacho
kitachunguza wale aliopewa viwanja wakati hawakuwa wakazi wa maeneo hayo,
ambapo kwa kushirikiana na vyombo vvya dola mkondo wa sharia utachukua nafasi
yake.
No comments:
Post a Comment