Tuesday, 27 February 2018
KAMATI YA MAADILI YAWAFUNGIA VIONGOZI MVUVUMWA KWA KUGHUSHI LESENI ZA WACHEZAJI
KAMATI ya Maadili ya TFF iliyokutana Februari
3, 2018 na Februari 17, 2018, katika ofisi za TFF Karume, pamoja na mambo
mengine yaliyojadiliwa pia ilipitia na kutoa hukumu ya tuhuma za kutoa taarifa
zisizo sahihi na kughushi leseni za usajili zilizowakabili watuhumiwa
mbalimbali walioletwa mbele yake.
Tuhuma hizo zilitokana na mechi namba 26
Kundi A ligi daraja la kwanza iliyofanyika Oktoba 29, 2017 kati ya Mvuvumwa FC
na Friends Rangers ambapo katika mchezo huo timu ya Mvuvumwa FC iliwachezesha
wachezaji watano (5) ambao ni Elias Costa Elias (jezi namba 5), Lukwesa Joseph
Kanakamfumu (jezi namba 7), Dunia Abdallah Dunia (jezi namba 1), Doto Justine
Kana (jezi namba 12) na Mwarami Abdala Mwarami (jezi namba 8).
Kamati imemtia hatiani kocha na mratibu wa
Mvuvumwa FC, Joseph Kanakamfumu kwa makosa yote mawili, kutoa taarifa zisizo
sahihi, (udanganyifu) ili kufanikisha usajili wa wachezaji kinyume na taratibu
za ligi daraja la kwanza.
Kosa la kwanza Kanakamfumu akiwa kocha wa
Mvuvumwa FC aliwaorodhesha wachezaji (Elias Costa Elias, Lukwesa Joseph
Kanakamfumu, Dunia Abdallah Dunia, Doto Justine Kana Mwarami Abdala Mwaram)
kushiriki mechi namba 26 huku akijua kwamba hawana leseni halali kutoka TFF,
wachezaji wote walitoka katika kituo ‘academy’ anayoiendesha hivyo ni dhahiri
alijua alichokuwa anakifanya.
Kosa la pili Kanakamfumu aliamua kuwaongeza
wachezaji hao baada ya kukabidhiwa timu kwa vile alifahamu uwezo wao na
inaonekana alitumia uzoefu wake katika mpira wa miguu kupata leseni za
kughushi.
Kwa makosa hayo, kamati inamfungia Joseph
Kanakamfumu kutojihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka
mitano.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment