JUMLA ya Sh milioni 293 zilikusanywa na Tume ya
Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti
Ukimwi (AIDS Trust Fund) katika hafla ya kuchangia iliyofanyika katika Hoteli
ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi katika harambee hiyo alikuwa Rais wa
Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa, ambaye pia alitunukiwa ulezi wa mfuko
huo, ambapo aliubali.
Akizungumza wakati wa ufungaji wa hafla hiyo,
Mkurugenzi Mkuu wa Tacaids, Dk Leonard Maboko aliwashukuru wote waliochangia,
ambapo alisisitiza kuwa hakuna senti hata moja itakayotumika vibaya.
Maboko alisema kuwa fedha hizo zitasaidia kusaidia
shughuli mbalimbali za mfuko huo katika mapambano yake ya ukimwi.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Tacaids, Nadhifa Omar (kushoto) na mratibu wa Harambee ya kuchangisha fedha za Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (Aids Trust Fund), Teddy Mapunda. |
Mkapa ambaye ndiye muanzilishi wa mfuko huo wakati
akiwa Rais na kutangaza Ukimwi kama Janga la Taifa, jana usiku alisema kuwa mfuko
huo umesaidia sana kutoa elimu kwa wananchi kuhusu tatizo la ukimwi na jinsi ya
kupambana nalo.
Wakati huohuo, Kampuni ya uchimbaji madini ya Geita
Gold Mine imechangia mfuko huo kiasi cha Sh milioni 100.
Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa akimkabidhi cheti mwakilishi wa GGM, Tenga Tenga katika hafla hiyo. |
Mwakilishi wa GGM katika hafla hiyo, Tenga Tenga
alikabidhi hundi ya thamani hiyo kwa Rais Mkapa.
No comments:
Post a Comment