Monday, 26 February 2018
Norway Bingwa jumla Olimpiki Majira ya Baridi 2018
PYEONGCHANG, Korea Kusini
NCHI ya Norway imetwaa ubingwa wa jumla wa
Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi huku Marit Bjorgen akishinda medali ya
dhahabu kwa mbio za nyika za wanawake za kilometa 30.
Brorgen alitwaa medali hiyo ya dhahabu katika
siku ya mwisho ya michezo hiyo iliyofanyika jijini hapa.
Norway imemaliza michezo hiyo ikiwa
imejikusanyia jumla ya medali 14 za dhahabu sawa na Ujerumani, lakini imepata
medali 39 kwa ujumla, ikiwa n inane zaidi ya Ujerumani.
Bjorgen, 37, amekuwa mchezaji mwenye medali
nyingi zaidi katika michezo hiyo ya mwaka huu kwa kushinda medali ya shaba ya
timu, ikiwa ni medali yao ya tano katika michezo ya Pyeongchang 2018 na ni ya
15 kwa ujumla.
Mdada huyo alishinda medali katika kila
m,chezo alioshindana katika Olimpiki ya mwaka huu.
Pia alishinda medali ya dhahabu ka katika
shindano la wanawake la mbio za kupokezana vijiti la 4x5, alipata medali ya
fedha katika kilometa 15.
Akishindana katika Olimpiki yake ya mwisho
baada ya miaka 16 ya kushiriki michezo, Bjorgen alimaliza akiwa na medal inane
za dhahabu, nne za fedha na tatu za shaba kutoka katika michezo mitano.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment