Na
Mwandishi Wetu
WAKAZI wawili wa jijini Dar es Salaam ambao ni
wachumba, Solomon Mwaigwisa na Magreth Richard wameibuka washindi wa shindano
la Harusi ya Ndoto Yako lililokuwa likiendeshwa na chaneli ya Maisha Magic
Bongo Dstv chaneli 160.
Wapenzi hao wameshinda zawadi ya ufadhili wa harusi
yao ya kifahari itakayofanyika jijini Dar Es Salaam mwishoni mwa April mwaka
huu. Pamoja na kushinda Harusi ya Ndoto
Yao, wawili hawa pia watapewa zawadi ya fungate kwa hisani ya hoteli ya kitalii
ya Voyager Beach iliyopo jijini Mombasa nchini Kenya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice-Tanzania, Maharage Chande. |
Washindi hao walitangazwa leo asubuhi katika kilele
cha Siku ya Wapendanao katika hafla iliyofanyika makao makuu ya MultiChoice
Tanzania jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na washindi hao.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa
MultiChoice Tanzania Maharage Chande amesema channel ya Maisha Magic Bongo
imeamua kuwatunuku watazamaji wake zawadi hiyo kupitia kipindi chake maarufu
cha Harusi Yetu kinachorushwa na channel hiyo ambacho huonyesha harusi
mbalimbali.
Kipindi cha Harusi Yetu kilianza kuruka Novemba 2016,
ambapo msimu wa pili wa kipindi hicho ulianza mwezi Julai mwaka 2017. Kipindi
hicho hurusha harusi mbamlimbali huku kikiangazia walikotoka wanandoa, hatua
wanazopitia katika mahusiano yao na hatimaye tukio la kufunga ndoa.
Kuanzia ilipoanza awamu ya pili Maisha Magic Bongo
ilianzisha shindano maalum lililojulikana kama Harusi ya Ndoto Yako ambapo
washiriki walikuwa wakijibu kuhusiana na kipindi cha harusi yetu ambapo kila
wiki kulikuwa na swali moja.
Waandishi wa habari wakifuatilia hafla hiyo. |
Baada ya usaili huu, Solomon mkazi wa Dar es Salaam
pamoja na mchumba wake Magreth waliibuka washindi na hivyo kupata zawadi ya
kugharimiwa harusi yao itakayofanyika jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 28
mwezi April mwaka huu.
Mfanyakazi wa DSTV, Shumbana. |
Akifafanua kuhusu zawadi hiyo, Maharage alisema
zawadi hiyo inamaanisha maharusi hao watarajiwa watagharimiwa kila kitu kuanzia
ukumbi, mavazi, chakula, vinywaji, burudani, pamoja na fungate la kukata na
shoka katika moja ya hoteli za kitalii Voyager Beach Hotel katika ufukwe wa
Mombasa nchini Kenya.
Wakizungumza katika hafla hiyo, Solomon pamoja na
mchumba wake Magreth wamesema wamefurahi sana kushinda na kutuzwa ufadhili wa
harusi yao. “Sote tunafahamu ni jinsi gani zoezi la harusi linavyokuwa na
patashika hususan kwenye suala la gharama.
Maharusi watarajiwa, Solomon na Magreth wakiingia stejini. |
“ Hivyo nafurahi sana na ninamshukuru Mungu kwa
kutuwezesha kushinda katika shindano la Harusi ya Ndoto Yangu kwani sasa sisi
kazi yetu ni kufikiria tu jinsi tutakavyoendesha maisha yetu kwani suala la
harusi limekamilika” alisema Solomon, ambaye ni Bwana Harusi mtarajiwa.
Ameipongeza Chaneli ya Maisha Magic Bongo kwa kubuni
shindano hilo ambalo lilileta msisimko mkubwa na kwamba anaamini kuwa channel
hiyo itaendelea kuimarika kwani kwa sasa imekuwa maarufu sana kwa kuwa ni
chaneli inayowafanya watanzania wajivunie vipaji vyao.
Bi Harusi Mtarajiwa, Magreth. |
DStv kupitia chaneli yake mahsusi ya maudhui ya
Kitanzania ya Maisha Magic Bongo imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha
kuwa tasnia ya Sanaa inakua na kuifanya iwe moja ya vyanzo muhimu vya mapato
kwa wasanii na hatimaye kuchangia katika uchumi wa nchi yetu.
Chanel ya Maisha Magic Bongo ilianzishwa tarehe 1
Octoba 2015, kwa lengo kuu la kuinua na kukuza vipaji na Sanaa hapa Tanzania na
pia kuongeza maudhui ya kitanzania kwa wateja wa DStv.
Maharusi watarajiwa wakati wa hafla hiyo. |
Kwa kipindi chote hiki Chaneli hii imekua kwa haraka
sana ambapo kwa sasa ni miongoni mwa Chaneli zenye watazamaji wengi zaidi
katika ukanda wa Afrika Mashariki. Chaneli hii imekuwa kitovu cha maendeleo ya
wasanii hapa nchini huku mamia ya wasanii wakipata fursa mbalimbali kutokana na
kazi zao kurushwa katika channel hii na pia kupata mafunzo na kipato kupitia
Sanaa.
Kwa upande wa tasnia ya filamu na uigizaji, Maisha
Magic Bongo imeleta mapinduzi makubwa na miongoni mwa filamu zinazotikisa
katika soko kwa sasa ni pamoja na Tamthila ya HUBA,ambayo ilipokelewa vizuri sana
na Watanzania, pia kuna filamu na vipindi vingine kama MWANTUMU, HARUSI YETU,
KITIMTIM pamoja na tamthilia mpya zilizoanza kuonyeshwa hivi karibuni za SARAFU
na KAPUNI ambazo zote zinazidi kuwa maarufu kila uchao.
Wedding Planner wa harusi hiyo. |
No comments:
Post a Comment