Marehemu Jerome Swai wakati wa uhai wake |
Tuesday, 27 February 2018
Wafanyakazi JNIA, TAA Wamlilia Swai
WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA) na wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA)
wamesikitishwa na kifo cha Bw. Jerome Swai (58) aliyekuwa fundi bomba mahiri
kilichotokea tarehe 26 , 2018 kwenye
hospitali ya Amana baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Wafanyakazi hao kwa nyakati tofauti walisema
marehemu Swai alikuwa hakubali kushindwa kwa kuhakikisha anatatua tatizo
linalohusiana na mabomba ya maji kwa wakati wote anapokuwa kazini.
Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa, Bi.
Hanna Kibopile alisema marehemu ameacha pengo kubwa kutokana na uchapakazi wake
uliotukuka.
Naye meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Mtwara,
Bw. Daimon Mwakyosa alisema marehemu alikuwa akifanyakazi kwa bidii na
hakukubali kushindwa.
“Marehemu alikuwa akiijua vyema kazi yake na
hakukubali kushindwa nakumbuka wakati nikiwa JNIA na tukiwa tumepangwa shift
(zamu) moja hakuna kilichoshindikana kwake kuhusu fani yake aliijua vyema kazi
yake,” alisema Bw. Mwakosya.
Bi. Fatma Matimba, Kaimu Meneja Utawala JNIA,
alisema marehemu Swai alikuwa mchapakazi, ambapo mwaka jana alichaguliwa kuwa
mfanyakazi hodari. Pia aliwahi kupewa cheti cha ufanyakazi hodari mwaka 2001
kinachotolewa TUGHE.
Marehemu Swai alizaliwa mwaka 1960 wilaya ya
Rombo, na kupata elimu katika shule ya msingi Kilesi mwaka 1976, na baadaye
kujiunga na Chuo cha Ufundi cha Makalema akisomea fani ya ufundi bomba daraja
la tatu, na baadaye kujiendeleza katika Chuo cha Ufundi cha Chang’ombe mwaka
1988 na VETA mwaka 2007.
Marehemu aliajiriwa na TAA mwaka 1984 akiwa kama fundi bomba daraja la
tatu na baadaye alijiendeleza na kufanikiwa kusoma hadi kufikia daraja la
kwanza. Marehemu ameacha mjane Bi. Honoratha Emmilian ambaye naye ni mfanyakazi
wa TAA katika Idara ya Utawala akiwa kama mhudumu.
Mungu aipumzishe Roho ya Marehemu mahala pema
peponi. Amina!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment