MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) itaongeza
pato lake kwa kiasi cha Sh milioni 253 kwa mwaka kutokana na ungezeko la tozo la
pango la ardhi watakalotozwa wapangaji katika Kiwanja cha Kimataifa cha Ndege
cha Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.
Hayo yameelezwa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri
ya TAA, Mhandisi Profesa Ninatubu Lema wakati akisoma taarifa ya wataalam
kuhusu mchakato wa vyanzo vya mapato katika Kiwanja cha JNIA kwa Waziri wa Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Makame Mbarawa.
Mhandisi Profesa Ninatubu Lema akisoma taarifa yake leo mbele ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Makame Mbarawa. |
Profesa Lema alisema kuwa ongezeko hilo la fedha ni
sawa na asilimia 35 mara baada ya kuanza kwa utekelezaji wa yalioyoridhiwa
katika majadiliano ya mikataba husika.
Alisema kuwa mikataba karibu yote ya TAA imetoa
mwanya wa kurejea tozo ya ardhi nay a tahafifi (review of land lease and
concession rates) kila baada ya miaka miwili, zoezi la majadiliano na watoa
huduma litakuwa endelevu na litakapofanyika litahusisha wataalam kutoka taasisi
nyingione, pale panapohitajika, kama ilivyofanyika mwaka huu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Makame Mbarawa (kulia) akizungumza leo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela. |
Taarifa hiyo ilihusu majadiliano yaliyofanyika na
watoa huduma/wafanyabiashara katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyerere yamevaa matunda baada ya baadhi ya maeneo kukubalika, ambayo ni pamoja
na ongezeko la tozo ya pango la ardhi (toka dola za Marekani 5.00 hadi 7.90) na
riba ya ucheleweshaji malipo ambayo ni asilimia moja.
Profesa aliongeza kusema kuwa timu hiyo ya wataalam pia
ilipendekeza tozo ya tahafifu kuwa kati ya asilimia 15 ya mapato ghafi kwa
mwaka.
Mbarawa aliipongeza timu hiyo ya wataalam kwa kazi
waliyofanya, lakini alisisitiza kuwa wapangaji wa kiwanja hicho wasinyanyashwe
na wale watakaozembea kulipa pango wasionewe huruma.
Alisema ni aibu kwa taasisi yenye uwezo wa
kujiendesha kwa kutumia vyanzo vyake, kupiga hodi serikali na kuomba omba fedha
kila siku.
Wakati
huohuo, Serikali imesema
mchakato wa uboreshaji wa Shirika la ndege la Tanzania(ATCL)
unaoendana na ununuzi wa ndege mpya
unaoendelea kufanywa na Serikali hivi sasa, umelenga kuliboresha shirika hilo
kwa lengo la kulikuza kibiashara ndani na nje ya Tanzania na hivyo kuliingizia
fedha na hivyo kukuza uchumi wa taifa.
Profesa Mbarawa aliyasema hayo leo baada ya
kutembelea ujenzi wa sehemu ya tatu ya jengo la abiria la JNIA (Terminal 3) unaotekelezwa
na Kampuni ya Ujenzi ya Bam International ya Uholanzi, ambao umekamilika kwa
takeibani asilimia 68.5 na unatarajia kukamilika Septemba mwaka huu.
No comments:
Post a Comment