MANCHESTER, England
KOCHA Claude Puel ana tumaini winga mahiri wa
Leicester Riyad Mahrez atajisikia fahari kurejea katika kikosi chake.
Mahrez ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Algeria,
mwenye umri wa miaka 26, hajaichezea timu hiyo tangu Januari wakati uhamisho
wake kwenda Man City uliposhindikana.
Mchezaji huyo bora wa kulipwa wa mwaka 2016
aliwasilisha ombo lake la uhamisho, na Alhamisi kocha wa Mbweha hao Puel
alithibitisha kuwa hatampanga katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu dhidi ya vinara
City.
"Nafikiri ni muhimu sana sasa kuangalia mbele,
“alisema Mfaransa Puel.
"Riyad ni mchezaji muhimu na anapenda soka.
Anapenda uhusiano mzuri na marafiki zake. Ana uhusiano mzuri na wachezaji
wenzake, “aliongeza.
"nafikiri ni muhimu katika kipindi hiki kigumu
kuwaweka wachezaji wote na klabu pamoja ili kuendelea na kazi ngumu uwanjai.
Njia bora ni kurudi nyuma na kufurahia soka.”
Mahrez alijiunga na Leicester akitokea klabu ya
Ufaransa ya Le Havre kwa ada ya pauni milioni 400,00 Januari mwaka 2014.
Alifunga mabao 35 na kusaidia kupatikana kwa mengine
24 katika mechi 127 alizocheza katika Ligi Kuu, na alitangazwa kuwa mchezaji
bora wakati Mbweha ho walipotangazwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu 2016.
No comments:
Post a Comment