LONDON,
England
SERGIO Aguero
amefunga mabao manne wakati Manchester City ikiendeleza ubabe wake katika
kilele cha msimamo wa Ligi Kuu ya England na kufikisha pointi 16 zaidi, huku Harry
Kane akifunga wakati Tottenham Hotspur ikiwachapa wapinzani wao wakubwa Arsenal
kwa bao 1-0 jana.
Manchester
City iliibuka na ushndi mnono wa mabao 5-1 katika mchezo huo uliotawaliwa na
washindi.
Baada ya
kuanza taratibu kipindi cha kwanza katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja
wa Wembley, Kane aliruka juu na kuifungia kwa kichwa timu yake akifunga kwa
mara ya saba katika mchezo wa saba wa wapinzani hao huku likiwa goli lake la 23
katika ligi hiyo msimu huu.
Spurs, ambayo
katika mchezo huo ungeweza kushinda mabao mengi kama ingekuwa makini, lakini
umahiri wa kipa wa Arsenal Petr Cech, ndio ulizuia timu hiyo kupata mabao
zaidi.
Kwa ushindi
huo, Spurs sasa imepanda hadi katika nafasi ya tatu wakati Arsenal iko pointi
sita tofauti na Liverpool katika nmafasi ya nne huku kikosi cha kocha Jurgen
Klopp kikiwa na mchezo mkononi.
Kwenye Uwanja
wa Etihad, Aguero na mkali Kevin De Bruyne, ambaye alisaidia mara tatu, waling’arawakati
Man City ikitoa kipigo kwa mabingwa wazamani wa England Leicester katika
kipindi cha pili na kuiwezesha timu hiyo kupata ushindi wa 23 katika ligi kati
ya 27 msimu huu.
"Nafikiri
tulicheza vizuri leo, vijana wamefanya vizuri sana na hasa Sergio Aguero
alikuwa mchezaji tofauti kabisa, “alisema Raheem Sterling, ambaye alifunga bao
la kwanza la Man City, alipozungumza baada ya mchezo huo.
AGUERO AISIYEZUILIKA
Mshambuliaji
huyo alikamilisha hat-trick yake kabla ya kufunga la nne, baada ya kupiga mpira
uliogonga mwamba na kutinga wavuni.
Mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 29 tayari ameshafikisha mabao 21 ya ligi msimu huu na kuwa
mchezaji wanne kufunga zaidi ya mabao 20 katika misimu minne ya ligi mfululizo.
No comments:
Post a Comment