Na Mwandishi Wetu, Arusha
RIADHA Tanzania (RT) limesema kuwa halitasita tozo za ada
mpya za mbio za marathon licha ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuzisitisha
hadi watakapokutana Machi 5 mjini Moshi.
RT katika taarifa yake iliyotoa jana imesema kuwa
imefedheheshwa na kusitishwa kwa matumizi ya ada mpya kwa waandaaji wa mbio za
marathon, ambapo imesisitiza kuwa uamuzi wake uliotolewa Septemba 16 mwaka
jana, unabaki pale pale.
Alisema kuwa hiyo njia ya RT kujitafutia vyanzo vya
mapato ili kutoitegemea serikali katika upatikanaji wa fedha.
“Tunasisitiza kuwa waandaaji wote kuhakikisha wanalipa
ada kulingana na makundi
yaliyopangwa na kujisajili kabla ya kuendesha matukio yao,”anasema
Gidabuday.
Anasema kuwa waandaaji wote wanatakiwa kulipa ada zao kwa
wakati na wapewea hadi Februari 28 wawe wamekamilisha malipo hayo kabla hawajachukuliwa
hatua kali.
Alieleza kuwa kuhusu uamuzi wa BMT kuitaka RT kukutana
pamoja na waandaaji wa mbio ni jambo ambalo halitawezekana kutokana na
kuwa Kamati ya Utendaji haitaweza kuhudhuria kikao hicho kilichoitishwa
Machi 5 mjini Moshi.
“Sababu ya kushindwa kuhudhuria ni kutokana na wito mfupi wa kikao hicho, ambapo wajumbe
wengi watakuwa wametawanyika sehemu mbalimbali kutokana na majukumu ya chama, ikiwemo kushughulikia kambi ya taifa,”aliongeza.
“Ikumbukwe kuwa
Chama cha Waandaaji wa Mbio sio mdau wa RT kwa maana hakitambuliki rasmi kwetu,wadau halali wa RT ni waandaaji
wa mbio ambao wamejisajili na kulipa ada,”alisema.
No comments:
Post a Comment