TEHRAN, Iran
WATU 66 wamekufa baada ya ndege ya abiria kuanguka Iran,
maofisa wa ndege hiyo wamesema.
Ndege hiyo ya Shirika la Ndege la Aseman, ilikuwa
ikifanya safari yake kutoka Tehran kwenda katika jiji la kusini-magharibi la Yasuj,
ilianguka katika milima ya Zagros.
Shirika la Misaada la Mwezi Mwekundi liituma timu yake ya
waokoaji kwenda karibu na eneo la tukio karibu na jiji la Semirom katika jimbo
la Isfahan.
Ndege hiyo ilianguka katika Mlima wa Dena, ikiwa ni
kilometa 22 kutoka Yasuj, taarifa ya chaneli ya Irinn iliripoti.
Ndege hiyo ilikuwa na jumla ya abiria 60, wawili walinzi
wa usalama, wawili wafanyakazi wa ndege na rubani pamoja na msaidizi wake.
"Baada ya kuitafuta katika eneo hilo, bahati mbaya
tulitaarifiwa kuwa ndege hiyo imedondoka. Na kwa bahati mbaya abiria wetu
wapendwa wote wamepoteza maisha.”
No comments:
Post a Comment