Conte mbioni kuifundisha timu ya taifa ya Italia
|
Antonio Conte
|
LONDON, England
KOCHA wa Chelsea Antonio Conte ndiye chaguo
namba moja la kuwa kocha wa timu ya taifa ya Italia, makamu wa rais wa
Shirikisho la soka la Italia, Alessandro Costacurta alibainisha jana.
"Bado hatujachagua lakini nafikiri Conte
ni mmoja wa makocha ambao wanaweza kufanya vizuri. “Miezi kadhaa iliyopita
niliwahi kuzungumza naye.”
Nyota huyo wazamani wa AC Milan Costacurta ndiye
aliyepewa jukumu la kumtafuta mbadala wa Gian Piero Ventura, ambaye alitimuliwa
baada ya timu ya taifa ya Italia kushindwa kufuzu kwa Kombe la Dunia.
Conte, 48, aliifundisha Italia kutoka mwaka 2014
hadi kucheza robo fainali ya mashindano ya Ulaya, Euro 2016 kabla hajachukuliwa
na Chelsea.
|
Roberto Mancini
|
Wengine wanaofikiriwa kuwa na uwezo wa
kuifundisha Italia ni pamoja na Roberto Mancini, Claudio Ranieri na Carlo
Ancelotti.
"(Conte) tayari anajua jinsi ya
kuifundisha timu ya taifa ya Italia wakati wengine bado hawajahi kuifundisha, “alisema
Costacurta.
|
Claudio Ranieri |
Conte aliiongoza Chelsea kutwaa taji la Ligi
Kuu ya England katika msimu wake wa kwanza wa kuifundisha, lakini kwa sasa
inashikilia nafasi ya tano katika msimamo wa ligi hiyo, pointi 19 nyuma ya vinara
Manchester City.
|
Carlo Ancelotti
|
Costacurta aliendelea kusema: "Hiyo
naina maana kuwa sitakuwa na furaha na Mancini au na Ancelotti – ingawa (Ancelotti)
anaonekana mwenyewe amejiondoa katika mbio za kuwania kuifundisha timu hiyo.
No comments:
Post a Comment