SERIKALI ya Mkoa wa Singida imetoa ardhi hekali 20 kwa Kamati ya Ollimiki Tanzania (TOC) kwa ajili ya kujenga kituo cha
michezo cha Olimpiki Afrika.
Watoto wakishiriki mbio za kilometa 2.5 wakati wa Siku ya Olimpiki iliyofanyika kitaifa mkoani Singida leo kwenye Uwanja wa Peoples mjini humo.
|
Nchimbi alitoa ahadi hiyo jana wakati wa maadhimisho
ya Siku ya Olimpiki iliyofanyika kitaifa mkoani hapa kwenye Uwanja wa Peoples
hapa, ambako washiriki walianza mbio na kumalizia kwenye uwanja huo.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania TOC), Filbert Bayi akizungumza na wana habari baada ya kumalizika kwa maazimisho ya Siku ya Olimpiki kwenye Uwanja wa Peoples mjini Singida.
|
Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi alimshukuru Nchimbi
na kusema kuwa ofa hiyo ataiwakilisha kwa wenzake akiwemo rais wa kamati hiyo,
Gulam Rashid na Kamati ya Utendaji ili kuona wanaipokeaje ofa hiyo.
Katika hafla hiyo mtoto wakike na kiume wenye umri
mdogo na mwanamke na mwanaume mwenye umri mkubwa zaidi, kila mmoja alizawadiwa
zawadi na Nchimbi iliyotolewa na TOC.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Rehema Nchinbi akicheza ngome ya Kinyaturu ya Misake. Kulia ni Katibu tawala, Angelina Lutambi.
Kwa upande wa watoto wenye umri mdogo zaidi
waliomaliza wa kwanza katika mbio zao za kilometa 2.5, Careen Msasu mwenye umri
wa miaka sita na Stephen Joshua mwenye umri wa miaka 8 ndio walitwaa sh 50,000
kila mmoja kwa kumaliza wa kwanza.
Bibi wa zaidi ya miaka 90 akipokea zaadi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Rehema Nchimbi baada ya kumaliza na mbio na watoto wadogo.
|
Kwa upande wa watu wenye umri mkubwa zaidi
walioshiriki mbio hizo, Vitus Mutake mwenye miaka 71 na Tatu Chungu mwenye umri
wa miaka 59, nao walitwaa sh 50,000 kwa kumaliza wa kwanza huku wakiwa wenye
umri mkubwa kuliko washiriki wengine wa mbio za kilometa tano.
Siku ya Olimpiki duniani imekuwa ikifanyika Juni kila
mwaka na kuadhimishwa na zaidi ya nchi 200 duniani, ambazo ni wanachama wa
Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC).
Siku ya Olimpiki mjini hapa ilianza kuadhimishwa juzi
kwa usafi wa mazingira ambao Nchimbi na viongozi wa TOC walisafisha mazingira
katika mitaa na maeneo mbalimbali ikiwemo shule ya msingi Mwenge na soko la
matunda.
No comments:
Post a Comment