BRUSSELS, Ubelgiji
ASKARI wa Ubelgiji wamempiga risasi na kumuua mtu mmoja anayedai kuwa
alikuwa akitaka kulipua stesheni ya treni mjini hapa, imeelezwa.
Mtu huyo aliuawa mara baada ya kuripotiwa kuwa alikuwa akiunganisha
vilipuzi na hakuna mtu mwingine aliyejeruhiwa katika tukio hilo.
Waendesha mashtaka walisema kuwa mtu huyo alikufa. Wanalichukulia tukio
hilo kama shambulio la kigaidi.
Machi mwaka 2016, watu 32 waliuawa katika shambulio la kigaidi mjini
hapa, tukio mabalo lilidai kutekelezwa na kundi la kigaidi la Islamic State
(IS).
Kwa mujibu wa gazeti la Ubelgiji la La Libre Belgique, liliwakariri
waendesha mashtaka, mtu aliyeuawa alikuwa amevalia vilipuzi.
Nicolas Van Herrewegen, wakala wa relwe, alisema alikwenda chini katika
stesheni, ambako alisikia mtu akipiga kelele.
"Baadae alikuwa akisema 'Allahu Akbar' na alitupa sanduku lake la
matairi, “aliliambia Shirika la habari la AFP.
"Nilikuwa nyuma ya ukuta wakati mlipuko mdogo ukitokea. Nilikwenda
chini na kuwataarifu wenzangu. Mtuhumiwa aliendelea kuwepo eneo hilo na baadae
hatukumuona tena.”
"Haukuwa mlipuko mkubwa lakini kishindo chake kilikuwa kizito, “aliongeza.
“Watu walikimbia huku na huko.”
Bwana Van Herrewegen akimuelezea muhusika huyo alisema alikuwa mtu mwenye
mwili uliojengeka akiwa na nywele fupi, akiwa amevali shati jeupe na suruali ya
jinsi.
"Niliona kama alikuwa na kitu fulani niliona waya, huenda alikuwa
amevalia vesti yenye vilipuzi, “alisema.
Mwanasheria Remy Bonnaffe, 23, alikuwa akisubiri treni alifanikiwa kupiga
picha ya moto huo mdogo baada ya mlipuko.
Aliliambia Shirika la Habari la Reuters kuwa watu waliokuwa karibu na
mlipuko huo hawakuumia na hakuna ukuta ulioharibika.
"Nina furaha kuwa hakuna mtu aliyeumia nan i wazi kuwa jaribio hilo halijafanikiwa,
limefeli, “alisema.
Arash Aazami ambaye aliwasili muda mfupi katika stesheni hiyo baada ya
mlipuko huo, alisema alikuta watu wa usalama, huku watu wengine wakikimbia
mitaani kusaka usalama…, “alisema.
No comments:
Post a Comment