Na Mwandishi Wetu
Kwa mara nyingine tena Watanzania wamepata
uhakika wa kushuhudia michuano mbalimbali mikubwa ya kimataifa baada ya DStv kupitia SuperSport kuingia makubaliano ya kurusha michuano mikubwa ya
kimataifa, ikiwemo michuano ya UEFA Euro 2020 pamoja na ile ya kufuzu UEFA Euro
2020 na pia michuano ya Ulaya ya kufuzu Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.
Pia kuna lulu nyingine kwa Watazamaji wa DStv
hasa washabiki wa kandanda kwani pia mashindano mapya ya Ligi ya UEFA
itakayoshindaniwa na timu kutoka nchi zote 55, ambazo ni wanachama wa UEFA.
Michuano hii pia itakuwa ikioneshwa katika
chaneli ya SuperSport.
Makubaliano haya yanawahakikishia Watazamaji
wa DStv kushuhudia michuano yote mikubwa ya soka kila msimu hadi mwaka 2022.
“UEFA inafurahi kuendelea na kuimarisha
uhusiano wake wa muda mrefu na supersport,” amekaririwa Guy-Laurent Epstein,
Mkurugenzi Mtendaji wa UEFA Events SA.
“Supersport ni mshirika wa miaka nenda
rudi wa UEFA na tunaimani kubwa kuwa SuperSport itaendelea kuwahakikishia Watazamaji matangazo ya kiwango cha juu na pia amsha amsha ya UEFA 2018-2022 kwa mamilioni ya watazamaji
wa mitanange hiyo barani Afrika – Kusini mwa Jangwa la Sahara.
UEFA Euro 2020, ni moja ya michuano
itakayokuwa na shamrashamra nyingi ikizingatiwa kuwa itakuwa inatimiza miaka 60
tangu kuanza kwa michuano hiyo. Michuano hiyo itafanyika katika miji 13 ya nchi
13 tofauti barani Ulaya.
Michuano ya kufuzu ya Ulaya (The European Qualifiers) itakuwa ya aina yake wakati ambapo nchi 55 zitakabana koo kuwania
nafasi 24 za kushiriki michuano hiyo. Michuano hii ya kufuzu itaanza Machi 2019
hadi Machi 2020.
“Hii ni mikataba mikubwa na muhimu sana,” alisema Gideon Khobane, Ofisa Mkuu wa SuperSport.
“Michuano ya Ulaya kwa
kawaida huwa na mvuto mkubwa sana kwa
watazamaji wetu hivyo kuyafanya moja ya mashindano muhimu sanan.
Tunaamini kuwa michuano hii inaendelea kuwa mikubwa na maarufu Zaidi hivyo bila
shaka ushirikiano wa Supersport na UEFA utaongeza chachu katika michuano hiyo.
Kwa maelezo zaidi tembelea kurasa za mitandao ya kijamii ikiwemo
Facebook, Instagram na Twitter @DStvTanzania
na Tovuti - www.dstv.com
No comments:
Post a Comment