Na Mwandishi Wetu
MAKAO Makuu ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imejionea
shughuli za uendeshaji za vitengo vyake katika siku ya kwanza ya Wiki ya
Utumishi wa Umma, ambayo itamalizika Juni 23.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Ramadhan Maleta jana alijionea shughuli
hizo zinazofanywa na vitengo vya mamlaka hiyo.
Akizungumza na wakuu wa vitengo katika ofisi ya Mkurugenzi wa Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam (JNIA), Maleta alisema kuwa tofauti na
miaka mingine, mwaka huu wiki hiyo inaazimishwa kwa kutembelea vitengo
mbalimbali ili kujua uendeshaji wake, changamoto na jinsi wanavyopambana nazo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Ramadhan Maleta akiteta na Kaimu Mkurugenzi wa Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA), Joseph Nyahende (kushoto) wakati wa kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma leo. Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu.
Alisema utaratibu huo umetolewa na serikali badala ya kufanya maonesho
kwenye Uwanja wa Taifa au katika viwanja vya ofisi mbalimbali, mwaka huu wiki
hiyo inaanzimishwa kwa wakuu kutembelea idara mbalimbali na kujionea utendaji
wa kazi na changamoto zinazowakabili.
Maleta alipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa JNIA, Joseph Nyahende
ambaye alieleza wanavyoendesha shughuli zao kuanzia kuwahudumia abiria na mambo
mengine mengi.
Pia Maleta alitembelea vitengo vya usalama katika eneo la kuwasili na
kuondokea abiria maarufu au VIP, ambako alipata maelezo kutoka kwa mkuu wa
usalama, Leonard Mbogom na kitengo cha uhasibu na kupata maelezo kutoka kwa
mhasibu msaidizi, Easter Mwigane
Msafara huo pia ulipitia katika vitengo vya Usalama, eneo la
kuondokea abiria katika Uwanja wa JNIA Terminal Two, kitengo cha makusanyo na kile cha
usalama kwenye uwanja huo.
Kitengo cha usalama kimekuwa na shughuli nyingi, ambapo kimekuwa kikiweka
kumbukumbu za idadi na muda wa ndege zilizotua na kupaa na usalama mzima wa
kiwanja na mambo mengine mengi.
Maleta alishukuru idara zote na kuzitaka kujitahidi kutatua changamoto
zinazowakabili, ambapo Jumatatu atakutana na wafanyakazi wote kuzungungumzia mambo mbalimbali zikiwemo kero.
No comments:
Post a Comment