Na Mwandishi Wetu
SERIKALI na Kamati ya Olimpiki Tanzania
(TOC) zimekutana na kujadili kwa kina kuhusu maandalizi ya Michezo ya Jumuiya
ya Madola itakayofanyika Gold Coast, Australia kuanzia Aprili.
Michezo ya 21 ya Jumuiya ya Madola
itafanyika Gold Goast kuanzia Aprili 4 hadi 15, mwakani, ambapo Tanzania
itakuwa miongoni mwa nchi zitakazoshiriki michezo hiyo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Harrison Mwakyembe na naibu wake, Anastazia Wambura juzi mjini Dodoma walikutana
na Makamu a Rais na Katibu Mkuu wa TOC,
Henry Tandau na Filbert Bayi, ambao walijadili kwa kina maandalizi ya Tanzania
kwa ajili ya michezo hiyo.
Bayi alisema kuwa majadiliano yao
yalienda vizuri, ambapo waliueleza ujumbe huo wa Serikali kuhusu mpango wa
maandalizi wa Diplomasia ya Michezo, ambao ungeziwezesha timu za Tanzania za
riadha, kuogelea, ngumi na mpira wa meza kupiga kambi nje ya nchi kwa ajili ya
maandalizi hayo.
Alisema tofauti na mwaka 2014 wakati wa
maandalizi ya Michezo ya Jumuiya ya Madola iliyofanyika Glasgow, Scotland,
Serikali iligharamia nauli na posho za wachezaji walioenda katika kambi katika
nchi za Uturuki, Ethiopia, China na New
Zealand kwa kutumia mpango wa Diplomasia ya Michezo.
Bayi
alisema TOC mwaka huu ndio itagharamia nauli na posho kwa wachezaji na makocha
watakaoenda kuiga kambi nje ya nchi kwa ajili ya kujiandaa na Michezo ya
Jumuiya ya Madola ya Gold Coast mwakani.
Alisema Mwakyembe ambauye aliingia hivi
karibuni katika wizara hiyo akichukua nafasi ya Nape Nnauye aliyeondolewa na
Rais Magufuli, alikua hana taarifa kuhusu mpango huo wakati TOC ilishasilisha
suala hilo maema wakati wa Nape.
Alisema Mwakyembe aliahidi kulifanyia
kazi suala hilo na TOC wana mpango wa kukutana na Waziri wa Mambio ya Nchi za
Nje, Augustino Maige, ili kuhakikisha timu ya Tanzania inapiga kambo haraka nje
ya nchi kwa ajili ya maandalizi ya michezo hiyo.
Tanzania katika michezo hiyo ya Gold
Coast inatarajia kupeleka timu za riadha, ngumi na mpira wa meza, ambazo
zinatarajia kupiga kambi Ethiopia, Cuba na China.
No comments:
Post a Comment