Na Mwandishi Wetu
MAKAO Makuu ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) itatoa tuzo
kwa mameneja wote watakaofanya vizuri katika utunzaji wa mazingira.
Hayo yalisemwa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Salim Msangi wakati
wafanyakazi wa mamlaka hiyo wakifanya usafi nje ya Uwanja wa Kimataifa wa Ndege
wa Dar es Salaam (JNIA) Terminal 3 kuadhimisha Siku ya Mazingira.
Siku ya Mazingira Duniani inafanyika kesho nchini Canada wakati kitaifa
itafanyika mjini Butiama mkoani Mara, ambapo Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Msangi alisema kuwa, aliwataka mameneja wa viwanja vyote nchini kutunza
mazingara, ambapo aliahidi kuwa atatoa tuzo kwa yule atakayefanya vizuri zaidi.
Fulana iliyobeba ujumbe wa Mazingira wa Mwaka huu. |
Alisema kuwa wafanyakazi wa viwanja vya ndege wamekuwa mstari wa mbele
kutunza mazingira miaka yote ili kuhakikisha jamii inaishi katika eneo salama.
Mbali na kufanya usafi wa kufyeka nje ya Terminal 3, pia wafanyakazi hao
wa TAA Makao Makuu, waliweka mbolea na kupalilia miti waliyopanda mwaka 2014
katika eneo la kufikia na kuondokea abiria la watu mashuhuri la VIP kwenye
uwanja huo eneo la Terminal Two.
Kila mwaka wafanyakazi hao wa TAA wamekuwa wakifanya usafi au utunzaji wa
mazingira katika maeneo tofauti tofauti.
Akifafanua kuhusu tuzo, Msangi alisema kuwa ataanzisha tuzo na
atakayeshinda atapewa tuzo hiyo itakayoshindaniwa na viwanja vyote kupitia
mameneja wao.
“Nitaanzisha tuzo na meneja atakayeshinda nitamzawadia na pamoja na
wafankaazi wake ili kuhamasisha viwanja vingie nao wafanye vizuri ili washindi
mwaka unaofuata, “alisema Msangi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Salim Msangi. |
Pia alizitaja shughuli zingine wanazofanya ili kutunza mazingira ni
pamoja na kudhibiti maji taka yanayotoka viwajani, ambapo wana mabwawa
yanayokusanya maji yote, ambayo yanakuwa trited na kuwa safi kwa ajili ya
matumizi mengine ya binadamu.
Alisema kuwa mbali na hiyo pia wana mfumo mwingine ambao hutenganisha
maji na mafuta ili kulinda mazingira, ambapo usalama wa anga unachangia karibu
asilimia mbili ya uchafuzi wa mazingira kutokana na ndege kutoa hewa ya ukaa.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege wakifanya usafi leo. |
Mkuu wa Kitengo cha Mazingira wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Jofta Timanya akihojiwa na ITV leo. |
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) baada ya kumaliza kufanya usafi leo nje ya jengo la Uwanja wa Kimataifa wa Ndege la Julius Nyerere (JNIA) Terminal Three leo. |
No comments:
Post a Comment