Na Mwandishi Wetu, Mwanza
TIMU za wasichana za mpira a kikapu za Mwanza na
Kilimanjaro zimeendelea kutamba katika Michezo ya Shule za Sekondari
inayoendelea mjini haa baada ya kutoa vichapo kwa wainzani wao.
Mwanza waliifunga Tabora kwa pointi 66-20,
katika mchezo uliofanyika kenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba jana
Jumamosi.
Timu ya Mkoa wa Kigoma wenyewe waliibuka
washindi baada ya kuwashinda wainzani wao kwa vikapu 20-14 wakati Katavi
ilisambaratisha Tabora kwa vikapu 36 kwa 28 huku Simiyu ilipoteza kwa vikapu 12
dhidi ya 14 vya Mtwara.
Kwa upande wa timu za wavulana, Iringa alijikuta
akiokea kichapo cha pointi 20-14 kutoka kwa Dodoma huku Kilimanjaro ikitamba
dhidi ya Njombe kwa vikapu 54-42,
Mtwara ilishinda 38-25 dhidi ya Ruvuma wakati
Pemba ilifunga Pwani kwa vikapu 33-32 huku Morogoro ikiisambaratisha Simiyu kwa
vikapu 59-03.Tanga iliifunga Katavi 25-9 na Mara ilifungwa na Ruvuma vikapu
34-33.
Kwa upande wake mratibu mkuu wa mchezo wa
mpira wa kikapu Haidari Abdul alisema michezo hiyo inaendelea vizuri na vijana
wanajitahidi kucheza kwa kujituma.
Alisema wadau mbali mbali wajitokeze kwa
wingi katika kuhakikisha wanakuja
kuchagua wachezaji wenye vipaji ili kukuza mchezo huo hapa nchini.
Kwa upande wa mchezo wa soka, timu ya Unguja
ilishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Mbeya huku bao hilo ekee likifungwa na Ibrahim
Hamad.
Unguja ndio inayoongoza katika msimamo wa
Kundi C ikiwa na pointi 12.
No comments:
Post a Comment