Kocha wa Juventus, Massimiliano Allegri. |
CARDIFF, England
FAINALI ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
inachezwa leo jijini Cardiff ambapo Real Madrid inaumana na Juventus huku ikiwa
ina nia ya kuweka historia ya kulichukua kombe hilo mara mbili mfululizo.
Read Madrid, mabingwa watetezi, ikitwaa kombe hilo itakuwa ya kwanza
kulichukua mara mbili mfululizo lakini iko katika wakati mgumu kutimiza ndoto
hiyo kutokana na ushindani wa Juventus inayong'arishwa na mshambuliaji Gonzalo
Higuain.
Tangu kuanzishwa kwa Ligi hiyo mwaka 1993, hakuna iliyowahi kushinda
kombe hilo mara mbili mfululizo zaidi ya AC Milan mwaka 1989 na 1990 lakini
wakati huo lilikuwa likiitwa European Cup.
Mshambuliaji hatari wa Juventus ya Italia, Gonzalo Higuain. |
Real Madrid chini ya Kocha Zinedine Zidane ilitwaa kombe hilo kwa mara ya
11 ilipoibuka na ushindi dhidi ya Atletico Madrid katika fainali ya msimu
uliopita.
Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane. |
Akizungumzia mchezo wa leo Zidane alisema kikosi chake kimejiandaa vema
na wachezaji wana hali nzuri.
Alisema imewachukua muda na nguvu nyingi kujiandaa kufikia hatua hiyo
muhimu na kuwa kwa sasa kilichobakia ni kuchukua ubingwa tu.
Juventus mara ya mwisho kushinda kombe hilo ilikuwa mwaka 2006 chini ya
Kocha Marcello Lippi. Tangu hapo imefungwa mara nne hatua ya fainali ikiwa ni
pamoja na ile ya mwaka juzi na Barcelona.
Real Madrid wakiwa mazoezini. |
Juventus inayoshiriki Ligi Kuu Italia, ni timu ya tisa kushinda Ligi Kuu
hiyo na Kombe la Ulaya na ni ya pili kufikia hatua hiyo tangu msimu wa mwaka
2009 na 2010, ambapo Inter Milan iliibuka mabingwa.
Kocha wa Juventus,
Massimiliano Allegri alipoulizwa hatua hiyo ya kucheza fainali alisema kuwa
hiyo ni hatua kubwa na ngumu kuifikia.
Alisema Juventus imeshapoteza fainali sita kati ya nane, ambazo timu yake
imewahi kucheza Ulaya. Alisema kuna Ligi ya Mabingwa moja tu kwa Ulaya nzima na
anaona kuwa amefikia hatua kubwa na ya muhimu zaidi kuongoza timu kucheza
fainali hiyo.
No comments:
Post a Comment