Na Mwandishi Wetu, Singida
WAKATI maadhimisho ya Siku ya Olimpiki Duniani yanafanyika kitaifa kesho mjini Singida, Mkuu wa Mkoa huo pamoja na viongozi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), leo walifanya usafi katika maeneo mbalimbali.
MKUU wa Mkoa wa Singida, Rehema Nchimbi pamoja na viongozi mbalimbali wa TOC walifanya usafi katika maeneo tofauti tofauti ili kuadhimisha Siku ya Olimpiki ambayo itafanyika kesho Jumapili.
Akizungumzia kuhusu Siku ya Olimpiki, Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki
Tanzania (TOC), Filbert Bayi alisema kuwa, Nchimbi ndiye atabariki
maadhimisho ya Siku ya Olimpiki kwenye Uwanja wa People uliopo mjini Singida.
Bayi alisema kuwa wanafunzi shule
mbalimbali za msingi na sekondari pamoja na watu wengine, watashiriki mbio hizo
za kilometa 2.5 pamoja na zile za wakubwa, ambazo zitakuwa za kilometa tano.
Maadhimisho ya Siku ya Olimpiki Duniani
yamekuwa yakifanyika Juni kila maka , ambapo mwaka jana yalifanyika mjini
Mtwara na mgemi rasmi alikuwa mkuu wa mkoa huo, Halima Dendegu na
kuwashirikisha wakuu wote wa wilaya za mkoa huo.
No comments:
Post a Comment