Na Mwandishi Wetu
Ile tamthilia kabambe ya Huba inayoonyeshwa
kupitia DStv katika chanel ya Maisha Magic Bongo inaendela tena baada ya
kumalizika kwa msimu wa kwanza wa tamthilia hiyo mwezi Machi mwaka huu.
Huu
ukiwa ni msimu pili, tamthilia hiyo ambayo imeainishwa kama moja ya tamthilia
maarufu zaidi ukanda wa Afrika Mashariki, imeanza kwa kishindo kutokana na
kuongezwa kwa vionjo na pia washiriki maarufu wa filamu hapa nchini.
Tamthilia ya Huba huigizwa hapa nchini na
waigizaji wa hapa hapa nchini, akiwemo
Rammy Gallis (Dev), Riyama Ali, Muhogo Mchungu, Grace Mapunda (Tesa) na
Aunt Ezekiel (Jojo) ambaye ni muigizaji mpya katika tamthilia hii.
Akizungumzia ujio wa msimu wa pili wa Huba,
Mkuu wa chaneli ya Maisha Magic
Bongo Barbara Kambogi amesema tangu kuanza kwa tamthilia hiyo ya
Huba Mwezi Novemba mwaka jana imefanikiwa kuliteka soko la tamthilia hapa
Afrika Mashariki na kuifanya kuwa moja ya tamthilia matata kabisa katika soko
la Afrika Mashariki.
“Kwa mara ya kwanza katika historia ya filamu
na hususan tamthilila Watanzania tumefanikiwa kuiweka tasnia yetu ya uigizaji
filamu katika ramani ya kanda ya Afrika Mashariki na bara zima kwa ujumla
kutokana na ufanisi wa tamthilia yetu ya Huba ambayo inatayarishwa hapa nchini
na kuigizwa na watanzania wenyewe” alisema Barbara.
Amesema kuwa kwa ufanisi uloonyeshwa na
tamthilia hiyo katika msimu wa kwanza, wanatarajia kuwa msimu huu wa pili
utakuwa wa kuvutia zaidi hasa ikizingatiwa kuwa waigizaji wote wameiva vizuri zaidi, vionjo vimeongezwa na pia waigizaji wengine wapya akiwemo Anti Ezekiel
ambaye ni miongoni mwa waigizaji maarufu hapa nchini.
“Sisi DStv, na hususan channel yetu ya Maisha
Magic Bongo, tulisikia kilio cha muda mrefu cha Watanzania wengi waliokuwa
wakitutaka kuongeza maudhui ya Kitanzania, na hatimaye tukaamua kuanzisha
chaneli maalum yenye maudhui kutoka Tanzania. Na sasa tunaendelea kuiboresha
chaneli hii ya Maisha Magic Bongo na maudhui yake kwa ujumla hivyo watanzania
wasiache kutazama chanel hii kwani ni yetu” alisema Barbara.
Tamthilia ya Huba katika chanel ya Maisha
Magic Bongo inapatikana katika vifurushi vyote vya DStv kikiwemo kile cha DStv
Bomba kwa shilingi 19,975 tu kwa mwezi kikiwa ni moja ya vifurushi vya bei
nafuu kabisa sokoni.
Msimu huu wa pili wa huba unatarajiwa kuendelea
kwa miezi kadhaa na tamthilia hiyo
huoneshwa katika chanel ya Maisha Magic Bongo (DStv 160) kila siku za Jumanne
na Jumatano saa moja na nusu usiku.
No comments:
Post a Comment