Qatar baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Asia kwa mara ya kwanza, abada ya kuifunga Japan kwa mabao 3-1 juzi. (Picha na Mtandao). |
TOKYO, Japan
WENYEJI wa Kombe la Dunia 2022 Qatar wametwaa kwa
mara ya kwanza kabisa taji la Asia baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1
dhidi ya mabingwa mara nne wa taji hilo Japan.
Mshambuliaji Almoez Ali alivunja rekodi ya mchezaji kupachika
mabao mengi katika mashindano hayo ya Kombe la Asia pale alipofunga bao lake la
tisa kwa kichwa katika mchezo huo wa fainali.
Abdulaziz Hatem aliiweka timu yake kuwa mbele kwa
mabao 2-0 baada ya kufunga kwa shuti la umbali wa kama meta 20 kabla Japan
haijafunga bao lao la kufutia machozi kupitia kwa Takumi Minamino akiwa ndani ya boksi.
Mabao yalikuwa 3-1 baada ya Akram Afif (mtoto wa kiungo
wazanmani wa Simba, Hassan Afif) kufunga kwa penalti baada ya mchezaji
anayeichezea klabu ya Southampton, Maya Yoshida kuunawa mpira katika eneo la
hatari.
Teknolojia ya VAR ilithibitisha kuwa beki huyo wa Southampton,
ambayo inajukana kama Watakatifu aliishika kwa makusudi mpira huo, ingawa picha
marudio za TV zilionesha kama aliushika kwa bahati mbaya.
Penalti hiyo ya Afif ilikuwa na maana kuwa mchezaji
huyo alifunga bao moja na kusaidia mara 10, ikiwemo mara mbili katika mchezo
huo wa fainali, wakati wa mechi saba za Qatar katika mashindano hayo huko Umoja
wa Falme za Kiarabu.
Kikosi cha kocha waQatar, Felix Sanchez kimecheza saa
10 na dakika nane bila ya kuruhusu bao hata moja katika mashindano ya mwaka huu
ya Asia kabla ya kufungwa na Minamino.
No comments:
Post a Comment