Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Grayson Mwaigombe (watano kushoto) baada ya
kupokea vikombe vya ushindi vya Mashindano ya Mei Mosi 2018 kutoka kwa Makamu
Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya Uchukuzi (USC), Hassan Hemed (wanne kulia) Jijini Dar es Salaam jana, Watatu
kulia ni Katibu wa klabu hiyo, Mbura Tenga. (Na Mpigapicha Wetu).
Na Mwandishi Wetu
KLABU ya Michezo ya Uchukuzi imekabidhi rasmi vikombe
vya ushindi wa michezo mbalimbali vya mashindano ya Mei Mosi 2018 yaliyofanyika
mwaka huu mkoani Iringa, ambako pia ilitwaa ubingwa wa jumla.
Makamu Mwenyekiti wa Uchukuzi Sports Club (USC),
Hassan Hemed ndiye aliyekabidhi vikombe
hivyo kwa Mkurugenzi na Utawala na Rasilimali Watu, Grayson Mwaigombe
aliyepokea kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi,Ujenzi na Mawasiliano
(Sekta ya Uchukuzi), Dk Leonard Chamuriho.
Katika hafla hiyo fupi iliyofanyi katika wizara
hiyo jijini Dar es Salaam, USC ilikabidhi jumla ya vikombe 13 ilivyovitwaa
katika Mashindano hayo ya Mei Mosi 2018, ambapo katika michezo iliyotwaa nafasi ya
kwanza iibeba jumla ya vikombe saba.
Katika nafasi ya pili, USC ilitwaa vikombe viwili vya
michezo ya netiboli na Kamba kwa wanawake, huku vikombe vya nafasi ya tatu
vilikuwa viwili, ambavyo ni vya Karata kwa wanawake na wanaume.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa USC Mbura Tenga, vikombe
ambavyo klabu yao ilipata kwa kutwaa nafasi ya kwanza ni pamoja na Mbio za
baskeli, bao, drafti na kuvuta kamba vyote kwa wanaume wakati kwa wanawake
ushindi wa kwanza ulikwenda katika michezo ya mbio za baiskeli, draft na bao.
Chamuriho aliipongeza klabu hiyo kwa kutwaa ubingwa
huo na kuwapa muda wa kuijenga zaidi klabu yao hiyo ili iweze kufanya vizuri
katika mashindano mengine.
Makamu Mwenyekiti wa USC, Hassan Hemed (kulia) akiwa na wajumbe wengine wa klabu hiyo wakimsikiliza mgeni rasmi. |
Timu ya Uchukuzi mwaka huu imefanya vizuri zaidi
tofauti na miaka ya nyuma na pia ilitunikiwa cheti cha ushiriki cha Mei Mosi
2018 kama mshindi wa jumla, huku Ofisa Habari Bi Bahati Mollel wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) alitunikiwa cheti maalum cha ushiriki kwa
kutambua usambazaji wa taarifa kwa vyombo vya habari.
No comments:
Post a Comment