Na Mwandishi Wetu
MULTICHOICE Tanzania,
Imetangaza washindi wanne waliokidhi vigezo katika shindano la
MultiChoice Talent Factory lilizinduliwa rasmi mapema mwezi Mei mwaka huu . Programu hii itawezesha jumla ya vijana 60
kutoka katika nchi mbalimbali barani Afrika kuweza kupata mafunzo ya filamu kwa
kipindi cha mwaka mmoja katika vituo vitatu tofauti, kimojawapo kikiwa nchini
Kenya (Nairobi) ambapo vijana hawa watakuwapo ifikapo tarehe 01 Oktoba mwaka
huu.
Mchakato mzima wa kupatakana kwa washindi hawa ulichukua
takribani muda wa miezi miwili ambapo kwa hapa nyumbani Tanzania tulipokea
maombi kutoka kwa vijana zaidi ya 160, yaliyofuatiwa na mchujo ulifanyika
tarehe 20 Julai Mwaka huu hapa Dar es Salaam Tanzania.
Ili kuhakikisha kuwa tunasaidiana na serikali katika mkakati wake wa kuifanya sekta ya ubunifu na sanaa kuwa moja ya mihimili ya uchumi wetu, MultiChoice imeanzisha programu hii na tumeanza na sekta ya filamu.
Vijana wa kitanzania waliofanikiwa kufudhu katika mchakato huu ni Sarah Kimario kutokea Dar es Salaam, Wilson Nkya kutoka Kigoma, Jamal Kishuli kutoka Arusha na Jane Moshi kutoka mkoa wa Kilimanjaro, alisema Ronald Shelukindo, Meneja Uendeshaji MultiChoice Tanzania.
Tumebarikiwa kwa vipaji vingi katika fani mbalimbali na bila shaka
tukiwekeza katika vipaji vya vijana wetu bila shaka tutafanikiwa kupanua wigo
wa ajira na uchumi wetu na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi
wa nchi yetu.
Amesema
mafunzo hayo yataanza rasmi mwezi Oktoba mwaka huu itawawezesha vijana hawa
wanne kutoka Tanzania kuungana na vijana wengine kutoka nchi mbali mbali za
Afrika katika vyuo maalum vya mafunzo ya utengenezaji wa filamu ambavyo
vitakuwa nchini Nigeria, Kenya na Zambia.
Kwa upande wao, washindi waliotangazwa kufudhu katika program hii
wametoa shukrani zao za dhati hususani kwa kampuni ya MultiChoice sambamba na
serikali ya Tanzania kwa ujumla. Akiongea katika hafla nhiyo,
Wilson Nkya mmoja
kati ya vijana waliopata fursa hiyo alisema kuwa “ Kipekee hii ni fursa
tuliyokuwa tukiisubiri kwa muda mrefu na tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa
Kampuni ya MultiChoice, serikali na jamii yote kwa ujumla. Tunaahidi kufanya kila liwezekanalo na
mtegemee matokeo chanya kutoka kwetu’, alimalizia Wilson.
No comments:
Post a Comment