Na
Mwandishi Wetu, Zanzibar
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson amewataka
wanafunzi kusoma kwa bidii na kupata matokeo mazuri ili kuzintendea haki juhudi
wanazofanya wazazi wao kuwasomesha katika shule nzuri zenye huduma bora.
Tulia
aliyasema hayo jana mjini hapa wakati alipokutana na wanafunzi wa shule za
Filbert Bayi. ambao wamekuja kwa ajili ya shughuli mbalimbali zikiwemo za
michezo na mafunzo.
Naibu Spika wa Bunge la Muungano, Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi na walimu wa Shule za Filbert Bayi mjini Zanzibar juzi. |
Alisema
wazazi wanaupendo mkubwa kwa watoto wao na kuhakikisha wanapata elimu bora
katika shule nzuri, hivyo wanafunzi hawanabudi kuonesha shukrani kwa kusoma kwa
bidii ili kupata matokeo mazuri, kwani hawana sababu ya kushindwa kufaulu.
“Nawatakia
kila la heri na sitarajii kabisa mwanafunzi apelekwe katika shule nzuri zenye
elimu bora, alafu ashindwe kufanya vizuru, “alisema Tulia huku akiwapongeza
walimiliki wa shule hizo kwa kuhakikisha wanafunzi wanapat mahitaji yote muhimu
pamoja na elimu bora.
Akizungumza
kwa niaba ya shule hizo, Mkurugenzi msaidizi wa shule, Elizabeth Mjema
alimshukuru Naibu Spika kwa kukutana na kuwatia moyo wanafunzi hao na kuahidi
kufikisha salamu hizo kwa wanafunzi wengine waliobaki shuleni pamoja na viongozi
wote wa shule hiyo.
Zaidi ya wanafunzi 198 wa shule za msingi na
sekondari za Filbert Bayi za Kimara na Mkuza Kibaha, wako kisiwani hapa kwa
mwaliko wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar (SMZ).
Baada
ya ziara ya mafunzo kwa kutembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria, wanafunzi
na walimu wa shule hizo, Jumamosi watashiriki michezo mbalimbali katika Uwanja
wa Amaan mjini hapa.
Kesho
Ijumaa wanafunzi hao wa shule za Filbert Bayi pamoja na walimu wao watatembelea
Baraza la Wawkilishi baada ya leo kutembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria
ikiwemo kisima cha chini kwa chini, pango la watumwa, fukwe ambako watumwa
walikuwa wakipitishiwa na kupandishwa majahazi baada ya kupigwa bei na
kupelekwa Uarabuni, maskani ya Sultani, Stone Town na Forodhani, ambako
walipata fursa ya kula urojo.
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Tulia Ackson (kulia) akiagana na Mkurugenzi Msaidizi wa Shule za Filbert Bayi, Elizabeth Mjema mjini Zanzibar jana. |
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Filbert Bayi wakiingia katika kisima cha chini kwa chini kilichopo Mwangapwani kisiwani Zanzibar leo. |
Baadhi ya walimu wa Shule za Filbert Bayi wakiwa ufukwe wa Bahari ya Hindi leo mjini Zanzibar. |
No comments:
Post a Comment