Na
Mwandishi Wetu
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, ameagiza Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala,
wakakague viwanja 537 vilivyotengwa maeneo ya Msongola, kwa ajili ya waliokuwa
wakazi wa eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam Jumanne wiki ijayo ili
kujiridhisha kama viwanja hivyo vipo na vinafaa.
Mhandisi Nditiye ametoa
agizo hilo leo Agostri 30, 2018, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwe
nye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ambapo
alieleza wasiwasi wake kuwa kampuni iliyopewa kandarasi ya kuwatafutia viwanja
wananchi hao haijatekeleza wajibu wake ipasavyo licha ya kuwa tayari imelipwa
kiasi cha shilingi bilioni 3.7.
“Nakuagiza Mkurugenzi wa
TAA, kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Wilaya Jumanne ijayo muende mkakague eno
hilo la viwanja 537 muone kama vipo kwa sababu kumekuwa na shida sana na hawa
wenzetu wa Tanzania Remix Centre nyinyi wenyewe mnajua, kuna shida
ya miundombinu, sasa lazime mjue eneo hilo linafikika, na viwanja hivyo
vinajengeka.” Alisema
Alisema Wananchi wako
tayari kushirikiana na serikali katika kuhakikisha upanuzi wa uwanja unakwenda
vizuri.
Kampuni ya Tanzania
Remix Centre ilipendekezwa na Manispaa ya Ilala na kupewa kandarasi
ya kutafuta viwanja kwa ajili ya makazi mapya ya wananchi waliokuwa wakiishi
eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo kulikuwepo na
mivutano kati ya Mamlaka na Wananchi ambapo baadhi yao walipeleka shauri hilo
mahakamani na hiovyo kufanya zoezi hilo la kuwahamisha wananchi hao kwenye eneo
hilo jipya kusuasua.
Rosemary Shimata, mwakilishi kutoka Tanzania Remix Centre. |
Hata hivyo akitoa
taarifa kwa Mhe. Naibu Waziri Nditiye, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja
vya Ndege Tanzania (TAA), Bw.Richard Mayongela alisema, Novemba mwaka jana, TAA
ilikutana na wadau wakiwemo wananchi, Manispaa ya Ilala, Ofisi ya Mkuu wa
Wilaya na Kampuni iliyoingia ubia na Manispaa ya Ilala katika kutafuta viwanja
kwa ajili ya wananchi hao.
“Mradi huu ulihusisha
upatikanaji wa viwanja 1,600 kwa mujibu wa mkataba wa awali ambapo fidia yake
ilipaswa kufanywa kwa awamu mbili ya watu 800, hata hivyo kwa mujibu wa sheria
kipinde kile ilitaka mwananchi apewe eneo lakini alipwe fidia pia.” Alisema na
kufafanua kuwa.
“Sasa wananchi wa Kipawa
na Kigilagila walilipwa fidia kwa mujibu wa sheria na kwao hakukuwa na tatizo,
kwa maana walipewa fedha taslimu na viwanja maeneo ya Pugu Mwakanga.” Alisema
Bw. Mayongela
Akieleza zaidi Bw.
Mayongela alsiema Baada ya kufanya tathmini, ilibainika kuwa wananchi wa
Kipunguni A na Kipunguni Mashariki ambapo kulikuwa na viwanja 1,186 baada ya
kufanya tathmini viwanja vilivyohitajika siyo 1,600, bali ni 1,186, kwa ajili
ya fidia ya wananchi wa maeneo hayo mawili na katika viwanja hivyo viwanja 537
serikali ilishatoa kiasi cha shilingi bilioni 3.7 ili kutekeleza zoezi hilo.
Sisi kwa kushirikiana na
mbia wa Mnaispaa ya Ilala yaani Tanzania Remix Centre, tukaandaa vile
viwanja na viwanja vile vimeshapatikana na kuanzia hivi sasa, viwanja hivyo
vitagawiwa kwa wananchi.
Aidha, katika hatua
nyingine, Mhe. Nditiye amesema wakati umefika sasa kwa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege, kuanzisha kitengo cha Estate ili kihakikisha viwanja vyake vyote nchini
vinakuwa na hati miliki.
“Naguagiza uunde kitengo
cha Estate kisichozidi watu 10 ili kihakikishe kila kiwanja kinachomilikiwa na
TAA kinakuwa na hati miliki na hii itaepusha migogoro na wananchi.” Alisema.
No comments:
Post a Comment