Na Mwandishi Wetu
MABINGWA wa Ligi Kuu Bara, Simba ksho wanaingia kwenye
mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa Ligi hiyo kuwakabili Tanzania Prison katika
mchezo utakaopigwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Simba inashuka dimbani kama Bingwa mtetezi baada ya
kutwaa kombe hilo msimu uliopita ikiwa na pointi 69 nyuma ya Azam waliokuwa na
58.
Simba inaingia uwanjani ikiwa na hali ya kujiamini
baadaa ya jumamosi iliyopita kutwaa ubingwa wa Ngao ya jamii na hasa uwepo wa
kikosi kipana chenye wachezaji wenye uwezo mkubwa.
Ni wazi kuwa Simba itapambana katika kuhakikisha
inapata pointi tatu kwani ilifanya jitihada za kutosha katika kujindaa na msimu
wa Ligi hiyo baada ya kuweka kambi ya wiki mbili nchini Uturuki.
Kocha wa timu hiyo Patric Aussems alisema kikosi
chake kimefanya maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo huo na kudai kuwa michezo
ya kirafiki ilikuwa ni kwa lengo la kuangalia sehemu zenye matatizo.
“Nimetumia michezo ya kirafiki kama maandalizi ya
Ligi Kuu nina imani na kikosi kilichopo,ila kuna wachezaji walipata tatizo na
kutolewa dhidi ya Mtibwa hivyo nitasikiliza ripoti na wengine
watatumika,”alisema Aussems.
Kocha huyo anaimani kuwa kikosi chake kitafanya
vizuri kwani pamoja na kukerwa na mbinu ya wachezaji wake kutumia mipira mirefu
aliahidi kulifanyia kazi suala hilo.
Michezo mingine ya Ligi hiyo itakuwa ni Ruvu Shooting
na Ndanda, Alliance na Mbao Fc,Coast Union na Lipuli ya Iringa, Singida na
Biashara Mara na mchezo mwingine ni Kagera Sugar na Mwadui ya Shinyanga.
No comments:
Post a Comment